CHELSEA YAKARIBIA KUMNASA ALEXANDRE PATO

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu nchini England Chelsea wanakamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Corinthians Alexandre Pato kwa kwa ada ya uhamisho paundi Milioni 7.


Awali Corinthians waliitaka Chelsea kutoa kiasi cha paundi milioni 12 Kumnasa mkali huyo wa mabao ambaye alishawahi kiitumikia AC Milan kwa mafanikio makubwa.

Mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye miaka 26 anatarajia kusaini mkataba wa miaka mitatu usajili ambao utamfanya mshambuliaji Loic Remy kuondoka klabuni hapo na Taarifa zinasema kuwa pengine atatimkia Russia katika klabu ya Spartak Moscow. 


No comments

Powered by Blogger.