SIMBA MPYA CHINI YA KOCHA MAYANJA YAZIDI KUNOGA YAMUADABISHA KIBADENI NA JKT YAKE, AZAM NAYO YATAKATA TANGA.
Mambo yanazidi kumwendea poa kocha mpya wa Simba Jackson Mayanja baada ya kupata ushindi wake wa pili leo akiifunga Jkt Ruvu ya Pwani kwa bao 2-0
Mchezo huo wa ligi kuu nchini Tanzania ulipigwa katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam dhidi ya Jkt Ruvu ambayo inafundishwa na mchezaji na kocha wa zamani wa Simba Abdallah Kibadeni
Simba ambayo inazidi Kuimarika ilipata mabao yake kipindi cha pili kupitia kwa Hamis Kiiza aliyefunga bao la kwanza kwa penati kabla ya Danny Lyanga hajafunga bao la pili akiwatoka mabeki na kipa wa JKT Ruvu na kufunga.
Huko Jijini Tanga Azam FC wakiwa katika ubora wao waliifunga Mgambo JKT bao 2-1 na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 39 pointi 3 mbele ya Yanga ambao watacheza kesho dhidi ya Maji maji FC

No comments