MAN UNITED KUMWACHIA VICTOR VALDES ATIMKIE UBELGIJI
Kipa wa Manchester United Victor Valdes anatarajia kujiunga na klabu ya Ubelgiji Inayoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo Standard Liege kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu.
Valdes mwenye miaka 34, alisaini mkataba wa wa miezi 18 wakati alipojiunga na Manchester United mwaka mmoja uliopita.
Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona ameshaichezea United mechi mbili tu na hakuna uwezekano wa kucheza tena katika kikosi cha United.
Baada ya dili la kujiunga na Besiktas kushindakana mwezi Agosti wakala wa kipa huyo anategemea mteja wake ataondoka mwezi huu Januari.
No comments