TATHIMINI LIGI KUU MZUNGUKO WA KWANZA, YANGA VINARA,TAMBWE ANAONGOZA UFUNGAJI, KAGERA YA MWISHO
Mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara umefikia tamati jana kwa timu zote 16 kukamilisha mechi zake 15 za mzunguko huo na wikiendi hii itapumzika kupisha michuano ya Confederations Cup ambayo bingwa wake ataiwakilisha nchi katika michuano ya confederation Cup barani Africa
Mabingwa watetezi Yanga SC wanaongoza msimamo wa ligi hiyo kwa kujikusanyia pointi 39 ikiwa imecheza mechi 15 imeshinda mara 12, Imetoka sare mara 3 na haijafungwa mchezo wowote mpaka sasa imeshafunga mabao 36 ikifungwa goli 5 tu
Azam FC wanakamata nafasi ya pili wakiwa na pointi 39 sawa na Yanga timu zote hizo zikiwa hazijafungwa na zimetoka sare mara 3 ila Azam imefunga magoli 30 na kufungwa magoli 10.
Simba SC ambao walianza kwa kusuasua sasa wamepata moto mpya wakiwa na pointi 33 katika nafasi ya tatu ikiwa imeshinda mechi 10 na kutoka sare mara 3 na ikifungwa mara mbili ikifunga magoli 23 na kuruhusu kufungwa mara 9.
Nafasi tatu za mwisho zinakamatwa na Kagera Sugar inayoshika mkia ikiwa na pointi 9 katika nafasi ya 16 sawa na African Sports wanaokamata nafasi ya 15 wakiwa pia na pointi 9 lakini Kagera wakiwa wamefungwa magoli mengi zaidi. Coastal Union wanakamata nafasi ya 14 wakiwa na pointi 10.
Kwa Upande wa wafungaji bora mpaka sasa Amiss Tambwe wa Yanga anazidi kuwakimbiza akimaliza mzunguko wa kwanza akifunga hat-trick dhidi ya Majimaji Yanga ikishinda bao 5-0.
Tambwe amefikisha jumla ya magoli 13 anafatiwa na Hamisi Kiiza wa Simba mwenye magoli 10, Donald Ngoma (Yanga), Elias Maguli (Stand United), Jeremia Juma (Prisons) hawa wote wana magoli 9.
Wenye magoli 7 John Bocco,Shomari Kapombe na Kipre Tchetche wote hawa kutoka Azam Fc huku Ibrahim Ajib wa Simba akiwa na mabao 6 wakati Atupele Green wa Ndanda ana magoli matano.
Hii ndiyo tathmini fupi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara mzunguko wa kwanza

No comments