TAMBWE APIGA HAT-TRICK YANGA IKITOA DOZI NZITO KWA MAJIMAJI YA KALLY ONGALA, MTIBWA YAAMBULIA SARE TANGA

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Tanzania bara Yanga leo Wametoa kipigo cha mbwa mwizi baada ya kuilaza Maji maji ya Songea bao 5-0.


Pambano hilo la ligi kuu Tanzania bara lilipigwa katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam lilishuhudia Yanga wakipata mabao yao kupitia kwa Amiss Tambwe aliyefunga mabao matatu huku Donald Ngoma na mwenzie Thaban Kamusoko wakifunga bao moja moja

Kwa matokeo hayo Yanga wamerudi katika uongozi wa ligi hiyo wakiwa na pointi 39 sawa na Azam fC ambao wanakamata nafasi ya pili huku Simba wao wakibaki katika nafasi ya tatu na pointi zao 33

Kutoka Mjini Kishapu wenyeji Mwadui FC waliifunga Kagera Sugar bao 2-1 anaripoti mwandishi wetu Alexander Sanga kutoka katika dimba la Mwadui

Mwadui walipata mabao yao kupitia kwa Jerry Tegete na Fabian Ngwanse wakati Kagera Sugar wao walipata bao la pekee kupitia kwa Babu Ally

Huko Jijini Tanga Mtibwa Sugar wakisafiri mpaka jijini humo walilazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji African sports.

No comments

Powered by Blogger.