LA LIGA: REAL MADRID YAPETA, BARCELONA YAVUTWA SHATI NA VALENCIA (VIDEO)

Nchini Hispania nako ligi kuu nchi humo maarufu kama La Liga imeendelea tena katika michezo kadhaa. Real Madrid walikuwa nyumbani kuivaa Getafe, Granada walikuwa tayari kuwakabili Atletico Madrid na Barcelona walikuwa nyumbani kupambana na Valencia.



Real Madrid imejinyakulia pointi tatu muhimu kwa kuifunga Granada mabao 4 kwa 1, magoli ya Madrid yalifungwa na Benzema akifunga mabao mawili, Bale na Ronaldo huku lile la Getafe likifungwa na Delgado.

Kwa ushindi huo Real Madrid imefikisha Pointi 30 na kushika nafasi ya Tatu nyuma ya Atletico Madrid wenye pointi 32 na Barcelona wenye Point 33

Mchezo wa pili ulikuwa ni kati ya Granada na A. Madrid, ambapo A. Madrid wameibuka na ushindi wa magoli 2 kwa 0. Magoli ya A. Madrid yakifungwa na Diego Godini na Antonio Griezmann

Barcelona imetoka sare ya goli 1 kwa 1 na Valencia magoli yalifungwa na Suarez kwa Upande wa Barcelona na lile la Valencia lilifungwa na Mina

HIGHILIGHTS ZA MECHI LA LIGA

Real Madrid 4-1 Getafe


Granada 0 - 2 Atletico Madrid


Valencia 1 - 1 Barcelona

No comments

Powered by Blogger.