CHELSEA NI ZAIDI YA MAJANGA YAPIGWA NA TIMU KIBONDE NYUMBANI


Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini England Chelsea imejikuta ikigombania kutoshuka daraja badala ya kupigania ubingwa kama wengi walivyoitabiria kabla ya kuanza msimu mpya.


Ikiwa nyumbani darajani jana ilijikuta ikichapwa bao 1-0 na vibonde waliopanda daraja msimu huu ya AFC Bournemouth bao la Glenn Murray dakika ya 80.

Chelsea ambayo ilicheza vizuri katika mechi hiyo ilishindwa kabisa kupenya lango la wapinzani na kuishia kutoka kapa katika mchezo huo ulioonekana ungetoa matokeo chanya kwa timu hiyo inayomilikiwa na Roman Abramovic tajiri raia wa Russia.

Kwa matokeo hayo Chelsea wamebaki na pointi zao 15 katika nafasi ya 14 huku Bournemouth wakipanda mpaka nafasi ya 17 wakiwa na pointi 13.


No comments

Powered by Blogger.