LIVERPOOL YAUNGANA NA MAN CITY NA CHELSEA KUMALIZA WEEKEND VICHWA CHINI


Liverpool leo iliungana na Chelsea na Manchester City kuwa kati ya timu zilizomaliza wikiendi hii kwa vichapo katika ligi kuu nchini England.


Ikiwa ugenini katika uwanja wa Sports Direct zamani ukijulikana kama St. James Park Liverpool walikubali kichapo cha bao 2-0 toka kwa wenyeji Newcastle United.

Magoli yote ya Newcastle yalipatikana kipindi cha pili juhudi za kiungo Georgino Wjnaldum ambaye alitengeneza bao la kwanza ambalo lilipelekea beki wa Liverpool Martin Skertel kujifunga huku akifunga bao la pili baada ya kupiga shambulizi la kustukiza langoni kwa Liverpool ambao walipanda kutaka kupata goli

Kwa matokeo hayo Newcastle wameweza kupata pointi 3 muhimu ambazo zinawafanya kufikisha pointi 13 ikishika nafasi ya 18 katika msimamo wa ligi hiyo huku Liverpool wakibaki na pointi zao 23 katika nafasi ya 7.

No comments

Powered by Blogger.