RATIBA CAPITAL ONE: MAN CITY NA CHELSEA ZAKWAA VIGINGI, ARSENAL NA MAN UNITED "MTEREMKO"


Ratiba ya Hatua ya nne ya kombe la Capital One imetoka baada ya kumalizika mechi za hatua ya tatu jana Usiku.

Mabingwa Watetezi Chelsea watakua ugenini tena kucheza na Stoke City pambano ambalo linaonekana kuwa litaleta upinzani mkubwa hasa baada ya timu zote hizo kuwa na upinzani mkubwa zinapokutana

Liverpool ambao wamepita kwa kushinda kwa mikwaju ya penati itakua tena nyumbani kucheza na timu iliyopanda daraja msimu huu ya AFC Bournemouth.

Manchester United baada ya kuibuka na ushindi wa bao 3-0 jana usiku itakua tena nyumbani kucheza na Middlesbrough.

Arsenal baada ya kuifunga Spurs 2-1 wao watasafiri kuivaa Sheffield Wednesday, Sheffield ambao jana waliwashangaza Newcastle United kwa kuwatandika bao 1-0 katika uwanja wa St. James Park.

Manchester City ambao juzi waliifunga Sunderland bao 4-1 watakua nyumbani kucheza na Crystal Palace mechi nyingine hii inayoweza kutoa matokeo yasiyotegemewa.

Mechi zote hizo zitachezwa kati ya Oktoba 27 na 28 mwezi Oktoba mwaka huu 2015.


RATIBA KAMILI CAPITAL ONE CUP RAUNDI YA NNE

Manchester City v Crystal Palace
Liverpool v Bournemouth
Manchester United v Middlesbrough
Everton v Norwich
Southampton v Aston Villa
Sheffield Wednesday v Arsenal
Hull v Leicester
Stoke v Chelsea

4 comments:

  1. Arsenal wameshinda 2-1 na man city walishinda 5-0 juzi hayo matikeo mlioandika sio sahihi bana

    ReplyDelete
  2. Arsenal wameshinda 2-1 na man city walishinda 5-0 juzi hayo matikeo mlioandika sio sahihi bana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hizza
      Man City walicheza juzi katika uwanja wa Mwangaza na kushinda bao 4-1 magoli ya Aguero,De Bryune, Sterling na kipa wa Sunderland alijifunga

      Kuhusu Arsenal hakuna tuliposema hawajashinda 2-1
      Asante

      Delete
    2. Hizza
      Man City walicheza juzi katika uwanja wa Mwangaza na kushinda bao 4-1 magoli ya Aguero,De Bryune, Sterling na kipa wa Sunderland alijifunga

      Kuhusu Arsenal hakuna tuliposema hawajashinda 2-1
      Asante

      Delete

Powered by Blogger.