SERIE A: MABINGWA JUVENTUS WANA HALI MBAYA KATIKA MSIMAMO

Mlinzi Leonardo Blanchard akishangilia bao la kusawazisha
Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Italia Juventus Bado inaonekana si lolote si chochote msimu huu baada ya jana usiku kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya timu iliyopanda daraja ya Frosinone.


Frosinone inakamata mkia wa msimamo wa ligi hiyo kwani tangu ligi ilipoanza na kuchezwa mechi 5 mpaka hivi sasa ilikua haijawahi kupata pointi yoyote na jana wakaweza kupata pointi yao ya kwanza dhidi ya makamu bingwa hao wa ligi ya mabingwa Ulaya msimu uliopita.

Juventus waliumiliki vilivyo mchezo wa jana lakini hawakufua dafu kwa safu ya ulinzi ya Frosinone ambao walicheza kwa nidhamu kubwa ugenini.

Simeone Zaza aliifungia Juventus bao dakika ya 50 ya mchezo baada ya kazi nzuri ya kiungo anayekipaga Juventus kwa mkopo akitokea Chelsea Juan Cuadrado goli ambalo lilidumu mpaka dakika 90 ambapo Leonardo Blanchard alifunga bao kwa Frosinone na kuzima kabisa ndoto za mashabiki wa Juventus kuibuka na ushindi.
Zaza akifunga bao la Juventus

Baada ya mechi 5 walizocheza mpaka sasa Juventus katika ligi kuu ya Italia wamefanikiwa kupata pointi 5 wakishinda mechi moja,wakitoka sare mechi mbili na kufungwa mechi mbili. Wanakamata nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na Inter Milan wenye pointi 15.

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA SERIE A JANA


  • Carpi 0-0 Napoli
  • Chievo Verona 1-0 Torino
  • Fiorentina 2-0 Bologna
  • Inter Milan 1-0 Hellas Verona
  • Juventus 1-1 Frosinone
  • Lazio 2-0 Genoa
  • Pallermo 0-1 Sasuolo
  • Sampdoria 2-1 As Roma 

No comments

Powered by Blogger.