RATIBA CAPITAL ONE: MAN CITY NA CHELSEA ZAKWAA VIGINGI, ARSENAL NA MAN UNITED "MTEREMKO"
Mabingwa Watetezi Chelsea watakua ugenini tena kucheza na Stoke City pambano ambalo linaonekana kuwa litaleta upinzani mkubwa hasa baada ya timu zote hizo kuwa na upinzani mkubwa zinapokutana
Liverpool ambao wamepita kwa kushinda kwa mikwaju ya penati itakua tena nyumbani kucheza na timu iliyopanda daraja msimu huu ya AFC Bournemouth.
Manchester United baada ya kuibuka na ushindi wa bao 3-0 jana usiku itakua tena nyumbani kucheza na Middlesbrough.
Arsenal baada ya kuifunga Spurs 2-1 wao watasafiri kuivaa Sheffield Wednesday, Sheffield ambao jana waliwashangaza Newcastle United kwa kuwatandika bao 1-0 katika uwanja wa St. James Park.
Manchester City ambao juzi waliifunga Sunderland bao 4-1 watakua nyumbani kucheza na Crystal Palace mechi nyingine hii inayoweza kutoa matokeo yasiyotegemewa.
Mechi zote hizo zitachezwa kati ya Oktoba 27 na 28 mwezi Oktoba mwaka huu 2015.
RATIBA KAMILI CAPITAL ONE CUP RAUNDI YA NNE
Manchester City v Crystal Palace
Liverpool v Bournemouth
Manchester United v Middlesbrough
Everton v Norwich
Southampton v Aston Villa
Sheffield Wednesday v Arsenal
Hull v Leicester
Stoke v Chelsea
Arsenal wameshinda 2-1 na man city walishinda 5-0 juzi hayo matikeo mlioandika sio sahihi bana
ReplyDeleteArsenal wameshinda 2-1 na man city walishinda 5-0 juzi hayo matikeo mlioandika sio sahihi bana
ReplyDeleteHizza
DeleteMan City walicheza juzi katika uwanja wa Mwangaza na kushinda bao 4-1 magoli ya Aguero,De Bryune, Sterling na kipa wa Sunderland alijifunga
Kuhusu Arsenal hakuna tuliposema hawajashinda 2-1
Asante
Hizza
DeleteMan City walicheza juzi katika uwanja wa Mwangaza na kushinda bao 4-1 magoli ya Aguero,De Bryune, Sterling na kipa wa Sunderland alijifunga
Kuhusu Arsenal hakuna tuliposema hawajashinda 2-1
Asante