CAPITAL ONE CUP: MAN UNITED,ARSENAL,CHELSEA MAMBO SAFI,LIVERPOOL CHUPUCHUPU


Wakati Manchester United,Arsenal na Chelsea wakiibuka na ushindi katika mechi zao za kombe la Capital One, Liverpool wao iliwabidi kusubiri mpaka penati kuweza kuwavusha hatua hii.


Man United ikiwa nyumbani iliweza kuifunga Ipswich town kwa bao 3-0 Magoli ya Wayne Rooney, Andreas Pereira na Antony Martial

Arsenal wao wakiwa ugenini dhidi ya wapinzani wao wa jadibTottenham Hotspurs waliweza kuibuka na ushindi wa bao 2-1 magoli yote mawili yakifungwa  na Mathieu Flamini huku Spurs wakipata bao lao kupitia kwa Calum Chembers ambaye alijifunga katika harakati za kuokoa mpira.

Chelsea ikiwa ugenini iliondoka na ushindi wa bao 4-1 wakiifunga Walsall magoli ya Chelsea yakifungwa na Loic Remy, Ramires,Kennedy na Pedro.

Liverpool wao walilazimika kusubiri mpaka muda wa penati ili kuweza kusonga hatua inayofata baada ya kulazimishwa sare ya bso 1-1 ndani ya dakika 90 dhidi ya Carlisle United na hapo ndipo Liverpool walipoibuka na ushindi wa penati 3-2.

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA JANA - CAPITAL ONE CUP


  • MK Dons 0-6 Southampton 6-0 
  • Crystal Palace 4-1 Chalton Athletic
  • Tottenham 1-2 Arsenal
  • Man United 3-0 Ipswich
  • Walsall 1-4 Chelsea
  • Newcastle United 0-1 Shelfield Wednesday
  • Norwich 3-0 West Brom
  • Liverpool 1-1 Carlisle **

No comments

Powered by Blogger.