LA LIGA : BARCELONA YAKUMBANA NA KICHAPO CHA HATARI


Katika hali ambayo haikutegemewa na Wapenda Soka wengi mabingwa wa Ulaya na Spain Barcelona wamechezea kichapo cha bao 4-1 wakiwa ugenini kwa Celta Vigo.

Mchezaji wa zamani wa wakali hao wa Catalunya Nolito alifunga bao la kwanza na kutengeneza mawili mengine kwa Iago Aspas na goli la nne lilifungwa na John Guidetti huku Barca wakipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Neymar. 

Hiki ni kipigo cha kwanza kwa Barcelona tangu kuanza kwa msiimu mpya wa ligi huku Celta Vigo ikipaa mpaka nafasi ya pili wakiwa na pointi 13 sawa na Real Madrid 

No comments

Powered by Blogger.