WACHEZAJI BORA WA DUNIA NILIOWAHI KUWAFUNDISHA NI WANNE TU ~ SIR FERGUSON
Kocha wa zamani wa Man United Sir Ferguson ameandika kitabu kipya ambacho ameeleza mambo mengi sana kuhusu Maisha yake kwa miaka 26 ndani ya Man United na hapa tumekuchambulia baadhi ya mambo yaliyomo katika kitabu hicho
- Fergie anakiri kuwa kabla hata man city hawajamnyemelea Sergio Aguero, Atletico Madrid waliiambia United itoe £35m kumpata Aguero lakin Fergie aliona pesa hizo ni nyingi na baadae akaenda Man city kwa £38m walikuwa desperate.
- Fergie anasema kwa mara ya kwanza waliambiwa na scouts kuna wonderkid aitwae Muller huko ujerumani na ana miaka 10, hivyo walitaka kumsajili ila muller aliamua kubaki academy ya Bayern.
- David Moyes alikuwa chaguo la 6 la Ferguson katika kuichukua united.Chaguo la kwanza lilikuwa Peo Guardiola baada ya kukutanaa naye Marekani wakati wa likizo.Mourinho alikuwa chaguo la pili ila alishampromise Abramovic kwamba angerejea,Klopp alikuwa chaguo la tatu ila alitaka kusign mkataba mpya dortmund.Ancelloti na Van Gaal walikuwa chaguo la nne na la tano but walikuwa na timu tayari huku ancelloti akiwa mrithi wa mourinho.Na hapo ndipo fergie na board wakaamua kumchukua Moyes.
- Fergie anasema dunia kwa sasa ina world class players wawili tu nao ni Messi na Ronaldo.na anasema amewahi fundisha world class playee wanne tu nao ni sholes,giggs,Ronaldo na Cantona.
- Fergie anasema alipinga upandishwaji mkubwa wa mshahara wa Rooney 2010 ambapo Rooney alisign miaka 5 na alikuwa akilipwa £180,000 ambapo ni mara mbili ya alchokuwa akilipwa Fergie..Ndipo Fergie akakutana na Joel glazer na kumwambia haiwezekani na wakakubaliana hakuna mchezaji atakayelipwa zaidi Ya SAF na ndipo SAF alipoongezewa mshahara.
- Mnamo mwaka 2010 Fergie alitaka kumsajili Balotelli ila washauri Fergie ndani ya Italia walimshauri Fergie kuwa ni risky sana kumsajili Balotelli kutokana na matendo yake.
- Fergie anasema Mino Raiola ndo alikuwa chanzo cha Pogba kuondoka man united coz walikuwa hawapatani na alijali pesa kuliko kipaji cha Pogba.
- Fergie anasema kosa kubwa la Moyes ilikuwa kuwafukuza staff nzima aliyoiacha na anampongeza Van Gaal kwa kumuweka giggs pale kwasababu anaijua vzuri club
- Fergie anakiri kuwa huwa anaangalia press conference za Van Gaal kwasababu zinashangamsha na kufurahisha.
- Fergie Anasema walikuwa karibu kumsajili Varane kabla Zidane hajaingilia kati na kumshauri aende Madrid.
- Fergie anasema wachezaji wa united walikuwa wakimrushia matani Ronaldo kwasababu alikuwa hawezi kupita mbele ya kioo bila kujiangalia...alikuwa ni mtu wa kujiangalia sana.
- Katika kipindi chake anasema watu wenye influence sana juu ya wachezaji wengine walikuwa ni Roy Keane,Bryan Robson na Steve Bruce.
No comments