TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA
DAVID DE GEA
Wakala wa kipa wa Man United David De Gea Jorge Mendes amekataa kupinga uwezekano wa kipa huyo kuhamia Real Madrid na kusema kila kitu kinawezekana.(Marca )
GABRIEL PAULISTA
Manchester United wanajiandaa kukuuteka usajili wa Arsenal kwa kumsajili beki wa Villareal Gabriel Paulista mwenye miaka 24 ambaye Arsenal wametangaza kuanza mazungumzo naye kutaka kumsajili.(Daily Star)
DOUGLAS COSTA
Chelsea wako katika mkakati wa kumsajili kiungo wa Shakhtar Donetsk mwenye miaka 24 Douglas Costa.(Sun)
DARREN FLETCHER
Bosi wa West Brom Tony Pulis amethibitisha kuwa anataka kuwasajili winga wa Wigan Callum McManaman na kiungo wa Manchester United Darren Fletcher, 30.(Times )
PATO
QPR wamepewa mshambuliaji wa Zamani wa AC Milan ambaye anaichezea Corinthians Alexandre Pato, 25.(Daily Mail)
RAHEEM STERLING
Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers anategemea winga wake Raheem Sterling mwenye miaka 20, atasaini mkataba mpya na klabu hiyo hivi karibuni.
. (Sky Sports)
AARON LENNON
Hull City wanamwania winga wa Totenham Aaron Lennon mwenye miaka 27 ambaye anajipanga kuondoka White Hart Lane mwezi huu.(Hull Daily Mail)
KEVIN DE BRYUNE:
Kiungo wa zamani wa Chelsea anayekipiga katika klabu ya Wolfsburg Kevin de Bruyne mwenye miaka 23, ambaye amehusishwa na kutakiwa na Arsenal na Manchester United amesema hana mpango wa kurudi katika ligi kuu ya England.(Daily Star)
CHICHARITO
Matumaini ya Mashambuliaji wa Man United Javier Hernandez (Chicharito) kusajili moja kwa moja na Real Madrid mara mkataba wake wa mkopo utakapoisha yameanza kufifia baada ya Real Madrid kuonyesha kutokua na uhitaji katika nafasi ya mshambuliaji na hii itamlazimu mshambuliaji huyo kurudi Old Trafford mwishoni mwa msimu.
(Daily Express)



No comments