ASAMOAH GYAN APELEKA MSIBA KWA ALGERIA
![]() |
| Gyan akishangilia bao alilowafunga Algeria |
Goli la Dakika za mwisho la mshambuliaji Asamoah Gyan lilitosha kuwapa ushindi Ghana wakiifunga Algeria ambao wanashikilia namba moja kwa ubora wa soka barani Afrika.
Mechi hiyo ya kombe la mataifa ya Afrika ilikua ni mechi ya pili kwa Timu hizo katika kundi C ilimalizika kwa Ghana kushinda kwa bao 1-0 huku wengi tukitarajia mchezo huo kumalizika kwa sare baada ya timu hizo kutoonyesha dalili za kufungana kabla ya Ghana hawajatumia njia ya kupiga mipira mirefu kuimaliza Algeria ambayo ilimaliza mchezo huo bila kupiga shuti lolote katika lango la Algeria.
Kundi C linazidi kuwa gumu baada ya timu tatu kuwa na pointi tatu kila moja baada ya Algeria,Senegal na Ghana zote kushinda mechi moja wakati Afrika Kusini Pekee ndo ambayo haijashinda mechi yoyote na inaingia katika mchezo wa badae leo kucheza na Senegal mchezo ambao Afrika Kusini wanatakiwa kushi. Kwa namna yoyote ile.

No comments