MBINU ZA LVG ZASHINDWA KUIPA USHINDI MAN UNITED
Akitumia mtindo wa diamond kocha wa Manchester United Luis Van Gaal alijikuta akishindwa kupata ushindi na kulazimishwa sare dhidi ya Cambriadge United katika kombe la FA.
Katika mechi hiyo ya raundi ya 4 ya kombe la Chama cha Soka Nchini England FA iliyopigwa katika dimba la Abbey ilishuhudia kikosi ghali kabisa katika Historia ya ligi kuu England kikilazimishwa sare ya bila kufungana na Cambridge United ambayo ni timu ndogo kabisa ya Ligi daraja la 2 na ikikamata nafasi ya 12 katika msimamo.
Licha ya kupiga pasi nyingi lakini zilionekana hazina maana yoyote baada ya kushindwa kabisa kuipita ngome ya Cambridge United huku mashuti kadhaa yaliyoelekezwa langoni mwa Cambridge United yakishindwa kuzaa bao
Kwa kutambua umuhimu wa mechi iyo kocha Luis Van Gaal aliweka kikosi kamili akiwemo kipa wake namba moja David De Gea, Phil Jones,Antonio Vallencia,Marcos Rojo,Daley Blind, Fellain,Januzaj,Di Maria, Wilson na Falcao.
Kwa matokeo hayo Man United itaialika Cambridge United katika mechi ya Marudiano kutafuta timu moja itakayoingia hatua ya 5 mechi hiyo itapigwa katika dimba la Old Trafford baada ya wiki mbili.




No comments