TANZANIA NA MAFANIKIO YA KUSADIKIKA
Watanzania nchini kote tumeungana
kushangilia na kufurahia mafanikio ya timu yetu ya taifa. Nikisema wote
namaanisha wadau wa soka hata wale wasiokua na mapenzi ya soka. Ni heshima kubwa
timu ya taifa imeleta ndani ya nchi yetu baada ya kufuzu kwenye mashindano ya kombe la dunia. Ni tukio la kihistoria ndani
ya nchi yetu,na hakuna mtanzania yeyote
atakayeusahau mwaka huu 2022. Kila kona ninayopita ni nderemo na vifijo,mabosi ofisini,wachuuzi
mtaani,wakina mama sokoni,wabunge bungeni wote wamejisitiri kwa nguo zenye rangi moja
zinazofanana.
Kila kona jezi za timu ya taifa zimevaliwa, Jezi ya timu ya taifa
imekua sare ya watanzania wote. Hakika kila jambo lina wakati wake, kuna wakati wa
kulia na kupata maumivu ya soka umeshapita, sasa ni wakati wa kufurahia matunda ya soka.
Napenda kuchukua fursa hii kumpongeza rais wa TFF wa sasa pamoja na
uongozi wote wa Soka la Tanzania. Nitakua mchoyo wa fadhila kwa kutokutambua mchango wa hali
na mali aliyeutoa mheshimiwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Rais wetu
wa awamu ya 6 kwa muda huu mfupi tangu ameingia madarakani amekua bega kwa bega na Tff pamoja
na wadau wote wa soka kuhakikisha
Tanzania tunahitimisha kiu ya safari ya kwenda Qatar tuliyokua tunaingoja kwa
muda mrefu. Napenda kuwashukuru wana habari wote nchini kwa kazi kubwa
waliyoifanya ya kuhamasisha watanzania kuishangilia timu yao ya taifa. Pia
napenda kushukuru makampuni yote Tanzania kwa mchango wao mkubwa wa fedha
waliotoa kuisaidia timu yetu ya taifa. Bila kusahau Kampuni kubwa Inayojishughulisha na Maswala ya Soka Tanzania WAPENDA SOKA CO.LTD
Dhumuni la makala hii ni kutoa pongezi za dhati kwa aliyekua rais wa TFF
bwana Jamal Malinzi sambamba na uongozi wote wa TFF uliokua chini ya bwana
Malinzi sambamba na uongozi wote wa serikali za awamu ya 4 na ya 5 ambayo ilikaa
madarakani kwa muda wa mitano tu lakini
ilifanya mambo makubwa na kukumbukwa na wapenda soka wote nchini na waTanzania kwa ujumla

Kwa kua bwana Jamal Malinzi aliamua kuweka nguvu zake zote kwenye timu
hii,aliamua kutengeneza akademi ya soka kwa ajili ya timu hiyo ya vijana
iliyochaguliwa. Vijana hao walianza kukaa pamoja mnamo mwaka 2015,pamoja na
mafunzo ya soka vijana hao walipata kuendelea
na masomo yao ambao wachache walikua wakimaliza elimu ya msingi na wengine
kuendelea na masomo yao ya sekondari kama kawaida.
Mnamo mwaka 2016 ndugu Jamal Malinzi aliamua kuhamisha kambi ya timu ya
taifa ya vijana na kuipeleka nchini Brazil,Vijana hao walikaa nchini brazil kwa
muda wa mwaka mmoja ambapo walipata nafasi ya kujifunza zaidi mbinu mbali
mbali za soka katika nchi hiyo ya kisoka
ya brazil. Mwaka 2017 timu hiyo ilirejea nchini na kuanza kushiriki michuano
mbali mbali ikwamo kutafuta nafasi ya kombe la dunia la timu za vijana chini ya
umri wa miaka miaka 20,Vijana hao
walikaribia kufuzu mashindano hayo ya Dunia lakini bahati haikuawa yao baada ya
kutolewa na Ghana katika hatua ya mwisho. Lakini Mungu si athuman timu hiyo
ilipata nafasi ya kushiriki mashindano ya mataifa ya afrika ya timu chini ya
umri wa miaka 20 yaliyofanyika nchini Misri. Timu hiyo ilitolewa na wenyeji
misri katika hatua ya nusu fainali, lakini ikafanikiwa
kulipiza kisasi kwa timu ya taifa ya Ghana baada ya kuifunga timu hiyo na
kukamata nafasi ya tatu katika mashindano hayo.
Macho na akili za
watanzania zikahamia katika timu hiyo ya vijana al maarufu future
generation. Makampuni mengi yakajitokeza kuidhamini timu hiyo ya taifa ya
vijana. Watu wengi wakawa na imani kuwa timu hiyo ndio mkombozi wa soka la
Tanzania. Mnamo mwaka huo huo 2017 uliitishwa uchaguzi mkuu wa Tff uliomrudisha
tena bwana Jamal Malinzi kuendelea kuiongoza TFF, Jamal Malinzi alipata ushindi
wa kishindo kwasababu ya kutekeleza sera zake zilizomuweka madarakani mwaka
2013 hasa sera ya kukuza soka la vijana.
Utaratibu wa kusaka vipaji kupitia
mashindano ya umiseta na umitashumta uliendelea kama kawaida. Mnamo mwaka 2018
timu ya taifa ya vijana(future generation) ilipelekwa nchini ufaransa chini ya udhamini wa makampuni
mbalimbali ambapo timu hiyo ilikaa kwa muda wa miezi tisa kabla ya kurejea na
kushiriki mashindano ya CECAFA yaliyofanyika nchini Kenya na kufanikiwa kufika
hatua ya fainali kabla ya mwaka unaofuta kushinda kombe hilo.
Timu hiyo iling’aa katika mashindano
mbali mbali barani afrika, lakini kubwa zaidi ni pale timu hiyo ilipofanikiwa
kufuzu mashindano ya Olympic 2020 mjini Tokyo na kufanikiwa kunyakua medali ya
dhahabu. Mwaka huo huo 2020 timu hiyo iliingia katika mechi za awali za
kufutafuta nafasi ya kucheza kombe la dunia,Tanzania chini ya bwana Jamal
Malinzi ilifuzu kuingia hatua ya makundi.
Siku ambayo haitasahaulika ni mwaka
2021 ambayo Tanzania ilikua ikitupa karata yake ya mwisho dhidi ya timu ya
taifa ya Nigeria, nakumbuka siku hiyo hakukuwa na kiingilio kuingia ndani ya
uwanja,uwanja wote ulifurika mashabiki na wapenzi wa soka kuishangilia timu ya taifa(Future
generation), nakumbuka ndio kwanza vijana hao walikua na wastani wa umri wa
miaka 23. Nigeria walikokua wanaongoza kundi hilo wakiwa na point 13 moja zaidi
ya Tanzania waliokua na point 12,Nigeria wakihitaji sare kuweza kufuzu kombe la
Dunia nchini Qatar huku Tanzania wakihitaji ushindi wa aina yeyote.
Sikumbuki ilikua dakika ya ngapi
ila nakumbuka ilikua mwishoni mwa kipindi cha pili beki mahiri na nahodha wa
timu hiyo aliruka kichwa kuunganisha kona iliyopigwa na kuiwezesha timu ya
Tanzania kwa mara ya kwanza kufuzu kwenye mashindano ya kombe la Dunia. Nderemo
na vifijo vilienea kila kona ya Tanzania.Siku hiyo ilikua sikuu kubwa kuliko
zote kuwai kutokea nchini mwetu.
Bwana Malinzi alimaliza muda wake
ndani ya mwaka huo huo 2021 na kuitisha uchaguzi mkuu wa TFF uliomuweka
madarakani rais wa sasa wa TFF. Lakini mafanikio haya yote ni maono ya bwana
Jamal Malinzi katika kuwekeza katika soka la vijana. Nakumbuka miaka ya 2013 na
2014 nilikua naandika sana makala kuhusu soka la vijana,sijui kama bwana
Malinzi kama alisoma au hakusoma makala hizo,Lakini ombi langu kubwa kwa yeyote
atakayesoma makala hii kama yupo karibu na bwana Jamal Malinzi ampelekee makala
hii asome pongezi zangu za dhati kwake.
Hakika 61 ina maana kubwa kwa
watanzania,Nchi yetu ilipata uhuru mwaka 1961 na bwana Jamal Malinzi akiwa na
miaka 61 aliiwezesha Tanzania kufuzu kombe la dunia kwa mara ya kwanza (mnamo
mwaka 2021 ambapo tulicheza mechi ya mwisho ya kufuzu),Na baadae mwaka
huu 2022 tutasherekea miaka 61 ya uhuru wa Tanganyika. Kama ilivyokua kwa hayati
baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere ndugu pia jamal malinzi
ni baba wa soka la Tanzania.
Na
Allen Kaijage a.k.a middle ya juu
0655106767
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Kweli hii ni ndoto, anything can happen as long as nia ikiwemo
ReplyDeleteKwa akili ya kawaida unaweza kudhani kuwa mwandishi ameandika hili kwa kujifurahisha kwani ameishi miaka mingi ijayo katika wakati uliopo. Ni kama unaangalia filamu ya matukio ya mwaka 2021 wakati wewe upo kwenye mwaka halisi 2014.
ReplyDeleteLakin kwa jicho langu la tatu mwandishi alikuwa na lengo maalumu la kutukumbusha jamii kuwa ili tuweze kufanya vizuri katika medani ya soka la kimataifa tunatakiwa tuwekeze kwa vijana. Ni vijana tu ndiyo watakao tutoa kwenye hichi kilio cha kushindwa na kutupeleka kwenye kilele cha mafanikio.
Nigeria walipotea kwenye anga za soccer, ila wakajiuliza na kuona walipokosea wakawekeza kwa vijana sasa wamerudi kwenye soka, Misri walitesa sana kwa sababu ya kuwekeza kwa vijana. Ghana walitikisa Africa na dunia nzima kwani waliwekeza kwa vijana
Brazili inajivunia kuwa na vijana wengi katika timu ya taifa, ujerumani vivyo hivyo, ubeligiji nd usiseme. Muda wa kuwatumia watu wenye miaka 28 - 29 (ya mpira umekwisha) sasa tuamke na kuwekezeka kwa vijana.
Asante mwandishi kwa kumkumbusha JAMALI MALINZI na kamati yake ya utendaji kuwa mafanikio ya nchi yetu yanategemea nguvu yetu ya kuwekeza kwa vijana. Kubadili jezi na jina la taifa ni nadharia tu tunahitaji mafanikio zaid ya kubadili jezi na jina la timu.
Muhsin hero