JAMAL MALINZI MKAZI WA MASAKI ADUI MKUU WA WAKAZI WA MANZESE
![]() |
Rais wa TFF |
Hakuna kitu kibaya kama kutembea
na mtu aliyeshiba wakati wewe una njaa,Shibe yake hua inampa hisia kuwa na wewe
umeshiba wakati minyoo inanguruma ndani ya tumbo lako.Hekima ya mtu mwenye
shibe haimfai mwenye njaa kama hekima ya tajiri isivyomfaa masikini.Katika
Dunia yetu mawazo ya tajiri ndio yanamtawala masikini.Hata sheria zote Duniani
zimewekwa kwa ajili ya watu wa tabaka la juu kuwatawala watu wa tabaka la chini.
Masikini hua hana thamani wala
nafasi ya kusikilizwa katika jamii yetu ya sasa hata biblia takatifu ilishasema kuwa “hekima ya masikini
hayasikilizwi”.Ndio maana kuna viongozi wachache sana maskini Duniani.Hata viongozi wa masikini ni
matajiri,masikini wameshakariri na kukubali bila kujali matokeo hasi yake.
Mfano kwenye bunge letu la
Tanzania wawakilishi wa wananchi wa manzese,mbagala,tandale wangekua wamevaa
uhalisia wa tandale,mbagala na manzese kusingekua na bajeti za kuumizana kama
hizi.Ila utakuta mwakilishi wa wananchi wa watu wa manzese anaishi
osterbay,mwakilishi wa wananchi wa tandale ananyumba kubwa masaki na mwakilishi
wa mbagala makazi yake yapo msasani,unafikiri hapo kitakachoendelea ni nini,
Kama si kiongozi huyo kuhisi maisha yake anayoishi masaki ni sawa na ya
wananchi wake wa tandale.
Pamoja na yote hayo kipo kitu
kimoja kinachowaunganisha watanzania masikini na matajiri,kitu hicho ni furaha
ya tajiri na masikini,shibe ya tajiri na masikini pia haki ya tajiri na masikini.Kiunganishi
hiko si kingine bali ni michezo haswa mpira wa miguu.
Mpira wa miguu unadumisha umoja
na mshikamano ndani ya nchi yetu.Haswa pale tunapokuwa tunaenda uwanjani kama
watanzania tukiwa na lengo na nia moja ya kuishangilia timu yetu ya
taifa.Kaijage nikiwa nimevaa jezi yangu yenye rangi za bendera ya taifa
niyoinunua shilingi 5000 manzese sokoni huku nikiwa na tiketi yangu ya shilingi
3000 mkononi huku nikiwa nimebaki na shilingi 2000 ya nauli itakayonirudisha
nyumbani kwetu gongo la mboto nikiwa ndani ya uwanja mmoja na Ridhiwani Kikwete
aliyekata tiketi ya shilingi 50,000 huku naye akiwa amevalia jezi iliyofanana
rangi na yangu ila ya kwake ameitoa zizou fassion wote ndani ya uwanja tukiwa
na lengo moja tu ya kuishangilia timu yetu ya taifa.Ni furaha ilioje kuwa na
mheshimiwa sehemu moja wote tukiwa tunawaza pamoja huku mioyo yetu ikitamani
kitu kimoja.
Sehemu kama hizo ndio sehemu
pekee watu wa lika tofauti,matabaka tofauti na nyazifa tofauti tunakutana kwa
pamoja tukiwa na lengo moja.Lakini kuna watu wachache wanaokosa roho za
uzalendo wanataka kuharibu umoja wetu pekee uliobaki. Asilimia chache ya walafi
wanataka kula raha zote za masikini. Nani asiyejua kua nchi yetu ni
masikini.?Nani asiyefahamu kuwa asilimia kubwa ya wananchi wa Tanzania wanaishi
kwa mlo mmoja?kwa umasikini wetu huo huo tunajibana na kujaza vibubu vyetu
tupate shilingi 3000 au 5000 ya kwenda kuishangilia timu yetu ya taifa.Kwa
umasikini wetu na mapenzi ya dhati kwa timu yetu mtu anatembea kwa miguu kutoka
mbeya mpaka dar es salaam kuja kuishangilia timu yetu ya taifa,Ni mapenzi ya
namna gani haya!
Lakini leo TFF ya bwana Malinzi imekuja na kiingilio kima cha chini
shilingi 7,000,bila shilingi 7,000 hakuna kwenda kuiona Taifa stars.Huu ni uonevu
kwa watu wa tabaka la chini. Kiwango hiki kitaleta ubaguzi na kuvunja umoja
wetu .Hapa sijui kigezo walichotumia kuweka kiwango hiki lakini kiwango hiki
hakiendani na hali ya nchi yetu pia soka letu.Hivi tungekua na kiwango kama cha
Nigeria,misri au Cameroon viingilio vyetu vingekuaje kama kwa mpira huu tu wa
ku unga unga kima cha chini cha kiingilio ni shilingi 7000?
Inasikitisha kwakweli,Kiwango hiki kitapunguza idadi ya washabiki
watakaoenda uwanjani kuishangilia timu ya taifa,na hamasa uwanjani itapungua.TFF
imeangalia faida watakayoipata bila kuangalia hasara itakayowapata.Sijui ni
nani ndani ya shirikisho letu anatoa ushauri kama huu.Unaweza kuweka kiingilio
hiki ukakosa vyote.Ukakosa washabiki pia
ukakosa fedha ulizotaka kukusanya.Katika pita pita zangu nimeuliza watu 25 wote wamesema hawawezi kulipa shilingi
7000 kwenda kuangalia mechi ya Stars huku wakitoa mawazo kiingilio cha chini
kinapaswa kiwe shilingi 5000 au chini ya hapo
Kwa hili TFF imechemka,TFF
inapaswa kuzingatia zaidi jinsi gani
timu yetu changa itakavyoweza pata matokeo ya ndani ya uwanja bila
kujali mapato.Nchi kama Zimbabwe iliweka kiingilio cha dola moja ambayo nia
sawa na shilingi 1600 za kitanzania ili kujaza rasilimali watu ndani ya uwanja
kuishangilia timu yao ya Taifa.Lakini TFF yetu nimetolea macho mapato ya
mlangoni kuliko matokeo ndani ya uwanja.TFF ingeweza kuweka kiingilio cha
shilingi 3000 na uwanja wa taifa ukafurika kuishangilia timu yetu changa ya taifa
kisha wakapata faida baada ya timu hiyo kufuzu mashindano ya Afrika.La sivyo TFF
itahamishia shilingi 3000 nyingi za watu zilizobidi ziende uwanjani kwenye
banda umiza za shilingi 500 kisha 2500 iliyobaki kuimalizia kwa futari kwa mama
ntilie.
Malinzi ameshindwa kutimiza ahadi yake aliyoitoa Tarehe 15 Mwezi Uliopita mara baada ya mchezo dhidi ya Zimbabwe na kuahidi kuwa kiingilio cha Stars kitakua kidogo mno kila mtu aweze kuingia kuishangilia timu kama walivyofanya Zimbabwe Swali hapa linabaki ahadi hiyo ni shilingi 7,000?
KAKA MALINZI KATIKA HILI UMECHEMKA
Malinzi ameshindwa kutimiza ahadi yake aliyoitoa Tarehe 15 Mwezi Uliopita mara baada ya mchezo dhidi ya Zimbabwe na kuahidi kuwa kiingilio cha Stars kitakua kidogo mno kila mtu aweze kuingia kuishangilia timu kama walivyofanya Zimbabwe Swali hapa linabaki ahadi hiyo ni shilingi 7,000?
KAKA MALINZI KATIKA HILI UMECHEMKA
NCHI MOJA ,HATIMA MOJA
KILA
LA HERI TAIFA STARS
Imeandikwa na Allen
kaijage jr aka middle ya juu
Kaijage jr @gmail.com
0655106767
No comments