MAMBO KUMI NILIYOJIFUNZA BAADA ROBO FAINALI YA KOMBE LA DUNIA
1. Kizuri walichonacho Ubelgiji ndo wanakikosa Costa Rica na kile bora walichonacho Costa Rica wanakikosa Ubelgiji. Ubelgiji wana wachezaji na Costa Rica wana timu. Miguu ya Hazard angevikwa De Bruyne japo kwa muda world cup hii Ubelgiji wangeweza kufika mbali.
2: Mchezaji bora mpaka sasa Uholanzi ni Arjen Robben. Ila kwa hatua ya nusu Fainali, Uholanzi watahitaji Van Persie aliye bora zaidi na Sneijder alie imara zaidi, ukimya wa hawa umewarudisha nyuma.
3: Colombia walimkosa kiongozi. Tatizo halikuwa mwamuzi, walicheza kwa presha wakiamini ile ilikuwa mechi ya wao kufuzu. Bahati mbaya waliingia kwenye mkumbo na akili ya wabrazil, kulipa kisasi cha faulo nyingi. Wangeyaepuka Haya wangepita.
4: Mathieu Valbuena.... Kama ungewatizama vyema Ufaransa ungejua dhahiri kwanini walitoka. Didier Deschamps alitegemea sana ubora wake, alipanga Ufaransa icheze vipi, aliamua amkimbize vipi Benzema, kukosa ubora wake dhidi ya Germany ilikuwa zaidi ya pigo kwao. Hili nalo ni tatizo kuwa na vijana wengi katika timu. Baada ya Germany kumzima huyu hawakuwa bora tena, Hata Pogba usingemwona, huyu anataka Pirlo awe safi ili akufurahishe, na halihitaji Valbuena aimarishe Ufaransa.
5: Joachim Loew kastuka kabla hakujakucha pengine tusingemwona hapo alipo. Ugonjwa wa Bayern alitaka kuuleta Ujerumani. Kumweka Lahm kiungo unaongeza akili nzuri ya ukabaji, ila sio nguvu ya kiungo. Soka la sasa linahitaji uwe imara kweli kweli katikati. Ndo maana wahuni kama Khedira na Alonso waliwashinda, Hata Muntari aliwasumbua sana, na imani Hata Matuidi na Cabaye wangewashinda sana. Schweinstiger alihitaji majukumu yake ili timu icheze. Loew alitoka ndotoni mapema.
6: Neymar.... Ndio watamkosa sana huyu Brazil lakini naona kama watamkosa zaidi Thiago Silva. Unahitaji kuuona ubora wa Luiz basi mweke pembeni kwa huyu, utulivu wa Brazil unaanzia kwa huyu, nguvu ya Brazil inaanzia kwa huyu, imani ya wabrazil ipo kwa Neymar ila uponyaji anao huyu. Sikushangaa kumwona Big Phil Scolari kukuna kichwa alipopata kadi ya njano. Aliliwaza hili.
7: Argentina, huitaji tingatinga la kumzuia Messi kuwafunga hawa. Unahitaji ubunifu katikati ya uwanja. Hawana ubora wowote hapo. Nina imani wanaomba Brazil amfunge Ujerumani kama watamfunga Uholanzi. Kibaya Wilmot wakati anamtoa Mirallas alimleta Mertens. Hakuepo Dembele pale? Alitakiwa kuja kushinda kiungo Tu. Yaani alitoa ndimu akaweka limau hakibadiliki kitu.
8: Ubora wa kocha unaanzia kwa ubunifu na kusoma akili ya mpinzani, Van Gaal alijua uchanga wa Costa Rica, kufanya mabadiliko ya goalkeeper ya goalkeeper lazima yaliwapa presha Costa Rica, walienda wakiamini wanatakiwa kuwa Makini zaidi, kuwa na ufundi zaidi katika matuta. Ukishapata hofu za hivi Una asilimia kubwa za kutoka. Sidhani kama lingekuwa tatizo sana kama wapigaji wa Upande wa pili wangekuwa akina Messi. Ila anaendelea kuniotesha huyu, nawaona Uholanzi wanacheza kwa imani ya kuwa na wao ni mabingwa.

10. Uholanzi vs Argentina. Shabaha Vs Uwezo. Wala huitaji akili ya Chuo kung'amua hili. Mezani Argentina wana uwezo mkubwa kuliko Uholanzi. Tofauti Yao ni Shabaha. Uholanzi Kuna kitu wamelenga, hawakutizami usoni, hawatizami unakuja vipi kuwaadhibu wanatizama eneo walilolenga. Ndio maana wapo hapo walipo, hawana timu bora Sana ila wanajua kupatia shabaha, wakipatia wamekumaliza. Udhaifu mkubwa wa Uholanzi ndipo ubora mkubwa wa Argentina ulipolalia. Defense vs Ushambuliaji. Vlaar vs Messi. Tatizo la Argentina ni shabaha, wanacheza kwa sababu wana uwezo sio kwa sababu wanastahili kufika Fainali. Muunganiko wao Una shida na unao tatiza. Ahsanteni.
By Nicasius Coutinho Suso (WS)
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
No comments