NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA NI UHOLANZI NA ARGENTINA,BRAZIL NA UJERUMANI (ULAYA VS AMERIKA KUSINI)
Mechi za mwisho za Robo Fainal Kombe la Dunia zimekamilika alfajiri ya leo kwa Uholanzi na Argentina kushinda mechi zao. Argentina ilishinda bao 1-0 dhidi ya Ubelgiji huku Uholanzi ikisubiri mpaka matuta kuwatoa Costa Rica kwa penati 4-3.
Kama ilivyotarajiwa na wengi michezo ya Robo Fainali ilikua migumu sana hata kwa timu zilizopita zilipita kwa ushindi wa tabu. Ukiangalia mechi ya kwanza kati ya Ujerumani na Ufaransa, Ujerumani ilishinda kwa bao 1-0 huku mchezo ukiwa mgumu sana muda wote shukrani kwa Goli la Mapema la Beki Matts Hummels.
Brazil nao walipata tabu kuifunga timu ngumu ya Colombia Brazil ikishinda kwa bao 2-1 magoli ya Brazili yakifungwa na Mabeki Thiago Silva na David Luiz wakati lile la Colombia likifungwa na James Rodriguez
Argentina wao walishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Ubelgiji bao la Gonzalo Higuain dakika ya 8 tu ya mchezo bao lililodumu kwa dakika zote 90 licha ya Ubelgiji kujitahidi vilivyo lakini haikuwasaidia.
Uholanzi wao ndo timu pekee ambayo imeingia hatua hii kwa mikwaji ya Penati baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 0-0 na hatimaye Uholanzi kushinda kwa penati 4-3.
Sasa tunaingia hatua ya Nusu fainali huku tukiwa na timu mbili za Amerika ya Kusini yani Brazil na Argentina pia tuna timu mbili za Ulaya Yani Uholanzi na Ujerumani hii inatupa taswira kwamba kuna uwezekani tukashuhudia fainali ya Ulaya na Amerika Kusini au Ulaya pekee kama sio Amerika Kusini pekee.
RATIBA YA MECHI ZA NUSU FAINALI
- BRAZIL vs GERMANY (Jumanne Saa 5 Usiku )
- UHOLANZI vs ARGENTINA (Jumatano Saa 5 usiku)
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
No comments