MAMBO KUMI NILIYOJIFUNZA MPAKA KUFIKIA HATUA YA 16 BORA KOMBE LA DUNIA
- Costa Rica wana nidhamu ambayo watanzania tumeikosa katika kunufaika na rasilimali zetu. Tuna Mlima mzuri zaidi, mbuga nzuri na madini ya kipekee lakini bado masikini, walau hawa wametumia vyema rasilimali zao chache, si ajabu wakifika mbali zaidi, ukitaka kuelewa maana ya nidhamu ya mpira watizame hawa.
- Kuna bahati kwenye mpira? Kama ipo basi anayo Brazil, acha nitamani mechi yao dhidi ya Colombia. Tatizo Lao linaanzia kwa Paulinho analihitimisha Fred. Scolari aliutegemea ule muunganiko wa Confederation, haupo tena.
- Messi, Messi, Messi, Messi. Ballon D'or 4, na Ronaldo yupo nje, Suarez hayupo, Zlatan Hata hakufika huku. Nani atamfunga paka kengele. Bado ni bora sana.
- Van Gaal analigeuza sikio kuwa kubwa kuliko kichwa. Pengine atafanikiwa na mwanga nauona. Kikosi kilichotakiwa kuchukua ubingwa ni kile kilichoenda kwa kina Tshabalala. Ila naona ndoto ya Van Bommel anaweza kuiota De Guzman, ajabu sana.
- Unataka kulijua tatizo la Spain, huhitaji ufundi mwingi, unaweza kuwatumia Bolt na Moh Farrah. Wakabe sana Kisha we kimbia, tatizo uti wa mgongo wao ni Tik Taka. Hata ukimtoa Xavi watamweka Alcantara au Koke. Wabadili mtizamo japo kidogo.
- Wakati mwingine sio vibaya ukajaribu kuota ama kuwaza yasiyotokea. Ni kheri Ramires au Henderson ndo wangekuwa wanastaafu Kisha Pirlo anachipukia. Atastaafu na kipaji chake, atazikwa nacho, pengine Hata mwanae hatokirithi. Bahati anacheza na Balloteli walau angekuwa na Messi.
- Cha msingi walichonacho Ghana wanakikosa Ureno. Na kikubwa walichonacho Ureno wanakikosa Ghana. Ghana wana,nidhamu ya mpira na Ureno wana Ronaldo.
- Januzaj 19, Hazard 22, Lukaku 21, Origi 17, Courtois 22, na wastani wa kikosi cha sasa ni miaka 25 wakitulia nusu fainali pale Urusi inawahusu.
- Thomas Muller...... Msimseme Miroslav Klose, huyu ana bahati na World Cup, anaweza kuja kuivunja Record ya De Lima mapema sana. Ahsanteni.
By Nicasius Coutinho Suso
No comments