KOMBE LA DUNIA - UJERUMANI YAINGIA NUSU FAINALI KWA MARA YA 13
Ikiwa katika kiwango bora kabisa na kuonyesjha kuwa nastahili kushika nafasi ya pili katika ubora wa Soka Duniani. Ufaransa imeweza kuibamiza timu ngumu ya Ufaransa kwa Bao 1-0 goli la Dakika ya 13 lililofungwa na Mlinzi wa Timu hiyo anayekipiga katika klabu ya Borussia Dortmund Matts Hummels akiunganisha mpira wa adhabu iliyopigwa kiufundi na Toni Kroos.
Licha ya kujitahidi kwa kiwango kikubwa kwa safu ya ushambuliaji ya Ufaransa walijikuta wakikwaana na kisiki cha Ujerumani kipa Manuel Neur ambaye alionekana dhahiri kuwa ndo nyota wa Mchezo huo.
Ujerumani wanaingia katika Nusu fainali yao ya 13 katika historia ya Kombe la Dunia ikiwa ni mara ya 4 mfululizo wanaingia katika hatua hii na kuifanya timu pekee iliyoweza kufikia mafanikio hayo.
Ufaransa kwa kufungwa leo imeendeleza Uteja kwa Ujerumani kwani haijawahi kuifunga Ujerumani katika kombe la Dunia tangu mwaka 1958
Je timu ipi itaifata Ujerumani Nusu fainali
Mechi inayofata ni Brazil vs Colombia ( Saa 5 usiku)
.... By Edo Daniel Chibo
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
No comments