UFARANSA NA UJERUMANI HAPATOSHI ROBO FAINALI LEO
Hatua ya Robo fainali ya kombe la Dunia Nchini Brazil inaanza leo kwa Mechi kali kati ya Ufaransa na Ujerumani kisha Brazil kuwakabili Colombia
Timu 8 ndizo zimeingia hatua hii huku Bara la Afrika na Asia kukiwa hakuna wawakilishi baada ya timu zao kuondolewa mapema.
mechi kati ya Ufaransa na Ujerumani inaonekana kuwa itakua mechi kali sana kutokana na timu zote kuwa katika hali nzuri wote wakiwa na viongo wenye macho na akili ya Mpira.
Brazil na Colombia ni mechi nyingine ambayo kutabiri matokeo ni ngumu sana kutokana na Ubora ambao Colombia wameuonyesha tangu kuanza kwa michuano hiyo.
Timu ambazo ziliongoza hatua ya Makundi ndizo zote zimeingia hatua hii ya Robo Fainali hivyo tunatarajia kushuhudia Robo fainali yenye ushindani wa hali ya juu.
Tumeshuhudia magoli mazuri na kila aina ya ufundi katika mechi zilizopita tangu tunaanza mashindano hayo huku Jumla ya magoli 154 yakiwa yameshafungwa.
Ratiba kamili ya hatua hii ya Robo fainali iko kama Ifuatavyo:-
- FRANCE vs GERMANY : Julai 4,2014 (Saa 1 Jioni)
- BRAZIL vs COLOMBIA : Julai 4,2014 (Saa 5 Usiku)
- ARGENTINA vs BELGIUM : Julai 5, 2014 (Saa 1 Jioni)
- UHOLANZI vs COSTA RICA : Julai 5,2014 (Saa 5 usiku)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
No comments