SAFARI YA AFRIKA KATIKA KOMBE LA DUNIA IMEISHIA HAPA



Timu mbili za Africa Algeria na Nigeria zimefuta kabisa ndoto za Waafrika kufika hatua ya Robo fainali katika michuano ya kombe la Dunia inayoendelea kule Brazil

Katika Mechi ya awali Nigeria ilikubali kichapo cha bao 2-0 toka kwa Ufaransa magoli ya Paul Pogba na lile la kujifunga la Mkongwe Joseph Yobo na kufuta kabisa matumaini ya Mabingwa hao wa Afrika kujaribu kufika japo Robo fainali kama walivyofanya majirani zao Ghana mwaka 2010.


Mechi hiyo ilichezeshwa na Mwamuzi Mark W. Geiger toka Marekani huku ikitazamwa na watazamaji 67,882.

Mechi ya pili ilikua kati ya Algeria na Mojawapo ya Timu inayopigiwa chapuo kuchukua Kombe la Dunia mwaka huu Ujerumani. Kwa Mshangao wa Wengi Algeria waliweza kuikabili vilivyo Ujerumani na kama si uhodari wa kipa wa Ujerumani Neuer basi kulikua na kila sababu ya kuamini kama Algeria wangeushangaza Ulimwengu.

Lakini Baada ya dakika 90 kumalizika bila Goli lolote ndipo zikaongezwa zile 30 ambazo zilizaa magoli matatu. Magoli Mawili ya Ujerumani yaliyofungwa na Mshambuliaji wa Chelsea Andre Schurlle na Mesuit Ozil  anayechezea Arsenal ya England. Huku Algeria wakizinduka katika dakika za nyongeza kwa kufunga goli pekee mfungaji akiwa ni Abdelmoumene Djabou.

Mechi ya Algeria na Ujerumani ilichezeshwa na mwamuzi Sandro Meira Ricci  toka Brazil na ilishuhudiwa na watazamaji 43,063.

TIMU ZILIZOINGIA HATUA YA ROBO FAINALI
  1. Brazil
  2. Colombia
  3. Uholanzi
  4. Costa Rica
  5. Ujerumani
  6. Ufaransa
Note: Zimebaki mechi mbili kukamilisha hatua hii 16 na mechi hizo ambazo zitapigwa leo Jumanne ni:-
  • Argentina vs Switzerland (Saa 1 jioni )
  • USA vs Belgium (Saa 5 usiku)

 +++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.