DAVID MOYES AKARIBIA KUPATA ULAJI UTURUKI


Aliyekua kocha wa Manchester United David Moyes Pengine atapata kibarua cha kuinoa Galatasaray ya Uturuki baada ya kuonekana akiwa katika mazungumzo na Viongozi wa klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu Nchini Uturuki.


Baada ya kumtimua kocha wake Roberto Mancini Galatasaray wanatafuta kocha mpya wa kuiongoza Klabu hiyo na katika orodha yao wapo makocha watatu Joachim Low (Kocha wa Timu ya Taifa ya Ujerumani), Jurgen Kliinsman (kocha wa Timu ya Taifa ya Marekani) pamoja na David Moyes ambaye hana timu baada ya kutimuliwa na Man United mwezi April.
Itampasa Moyes kusubiri mpaka kombe la Dunia Kuisha ili ahakikishiwe kama atapata kazi hiyo au hapana.


+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.