"SIKUMNG'ATA ILA MENO YANGU YALIJIGONGA BEGANI KWAKE" ~ LUIS SUAREZ




Mshambuliaji wa Liverpool na timu ya Taifa ya Uruguay ametoa utetezi wake kuhusu tukio la Kumng'ata beki wa timu ya Taifa ya Italia Georgio Chiellini na kusema kuwa hakudhamiria kumng'ata ila ilitokea bahati mbaya kwa uso kujigonga begani pake na meno kumjeruhi beki huyo na ndo mana baada ya tukio hilo alionekana ameshika meno kwani aliumia pia.


Suarez alitoa utetezi huo kwa Kamati ya maadili ya FIFA iliyoandikwa Tarehe 25 Juni 2014. "Najua mengi yamesemwa kuhusu tukio husika lakini nasisitiza sikudamiria kumng'ata Chiellini. Baada ya purukushani uwanjani nilipoteza balansi na kujigonga katika bega la Chiellini nikimuumiza kidogo na mimi kupata maumivu makali katika meno yangu" Alisema Suarez.

Jopo hilo la FIFA lilitupilia mbali utetezi huo na kumfungia huku wakisema "Suarez alidhamiria na kuna kila sababu ya kuhakikisha hilo" hivyo basi mkali huyo wa kupachika mabao sasa atatumikia kifungo cha miezi minne kutojihusisha na maswala yoyote ya Soka huku pia akiwa amefungiwa mechi 9 za kuchezea timu yake ya Taifa. Suarez pia amepigwa faini ya Paundi 66,000.

Je unadhani Suarez anadanganya?

~ Imeandikwa na Edo Daniel Chibo

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.