KOMBE LA DUNIA ~ WATALII SPAIN, CAMERUNI NA AUSTRALIA WAFUNGISHWA VIRAGO BRAZIL.
Michuano ya kombe la unia Mwaka 2014 litashuhudiwa kupatikana kwa Bingwa mpya kabisa baada ya mabingwa Watetezi Spain kutupwa nje kwa kufungwa mechi mbili jumla ya magoli 7-1 wakianza kufungwa na Uholanzi 5-1 kisha jana kufungwa 2-0 na Chile.
Spain Walianza kwa kasi mchezo wa Jana wakitegemea kupata chochote lakini wakajikuta wakipigwa 2-0 magoli ya Eduardo Vargas dakika ya 20 na lile la pili likifungwa na Charles Aranguiz na kuifanya Spain kuaga michuano hiyo mapema hata kama watashinda mechi ya mwisho dhidi ya Australia.
Mapema hiyo jana katika mchezo mwingine wa kundi hilo la B ulishuhudia Uholanzi ikishinda kwa bao 3-2 na kujihakikishia kuingia hatua ya pili ya michuano hiyo mikubwa kabisa Duniani.
Uholanzi ikipata magoli yao kupitia kwa Arjen Robben, Robin Van Perse na Memphis Depay huku Australia wakiungana na Spain katika kundi hilo kuaga mashindano hayo baada ya kufungwa mechi ya Pili huku ikibakiza mechi dhidi ya Spain ambayo hata kama watashinda hakuna watakachopata.
Kwa Upande mwingine Wawakilishi wa Afrika Cameruni walitangulia kuongoza safari ya kurudi Afrika baada ya kumaliza "Utalii" wao huko Brazil walipokubali kipigo cha pili mfululizo cha bao 4-0 toka kwa Croatia huku wakionekana kabisa ni timu ambayo ilienda kupoteza muda tu Brazil.
Alex Song alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kwa makusudi mchezaji wa Croatia pia mabeki wa Cameruni walionekana wakipigana wao kwa wao.
Magoli ya Croatia yalifungwa na Ivica Olic dakika ya 11, kisha Ivan Perisic dakika ya 48 na Magoli mawili ya mario Mandzukic dakika ya 61 na 73.
RATIBA YA MECHI ZA LEO
- Colombia vs Ivory Coast (Saa 1 usiku )
- Uruguay vs England (Saa 4 Usiku )
- Japan vs Greece (Saa 7 usiku)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
No comments