KWA TAARIFA YAKO ~ HAWA NDO WAFUNGAJI BORA KABISA KATIKA HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA



Fainali za Kombe la Dunia zinaendelea kule Brazil kwa magoli kufungwa kila kukicha na mpaka sasa Robin van Perse,Neymar na Robben wanaongoza katika listi ya wafungaji mwaka huu wakiwa tayari na goli mbili kila mmoja.

KWA TAARIFA YAKO tu wafuatao wamebaki katika vitabu vya kumbukumbu kutokana na kufunga magoli mengi katika historia ya kombe la Dunia:-
  • Edson Arantes do Nascimento maarufu kama Pele - BRAZIL
Akichezea Timu ya Taifa ya Brazil ameweza kufunga Jumla ya magoli 12 katika mechi 14.

  • JUST  FONTAINE - UFARANSA
 Akiichezea timu ya taifa ya Ufaransa aliweza kufunga jumla ya magoli 13 katika mechi 6 tu alizocheza

  • GERD MULLER - GERMANY
Mkali wa kupachika mabao wa timu ya taifa ya Ujerumani amefunga magoli 14 katika mechi 13


  • MIROSLAV KLOSE - GERMANY
Mkali huyu wa timu ya Taifa ya Ujerumani amecheza mechi 19 na kufunga magoli 14.

  • RONALDO DE LIMA - BRAZIL
Ronaldo anakamata nafasi ya kwanza kwa wachezaji waliofunga magoli mengi. Amefunga jumla ya magoli 15 katika mechi 19 alizoichezea Brazil.

 
tukutane katika Makala nyingine kama hii Jumatano
 
By Muhsin Siraji (WS)

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.