KWAHERI ADEN RAGE,KAMA TUKISAHAU TUTAKURUDISHA TENA KWA MATARUMBETA
Binadamu
tumeumbwa kusahau Yani utashangaa Leo tunalia ,kesho ikifika tunacheka kidogo tunasahau kilio
cha jana. Ndivyo tulivyoumbwa wanadamu,ndivo tulivyo Waafrika,Wazungu na Waarabu pia. Umeshajiuliuza
tusingeumbwa kusahau ingekuaje? Labda
tusingeumbwa kusahau tungeumbiwa roho za chuki na visasi mioyoni
mwetu.Labda tusingeumbwa kusahau tungejikinga na vitu vilivyotuletea simanzi
jana ili tusipate huzuni tena kesho.sijui jibu sahihi ni lipi kwako Mtanzania. Mtanzania
wewe wanaekulaghai kwa miezi 6 ili uwe mtumwa wa miezi 54,hii yote haya kwasababu
umeumbwa kusahau.
Watanzania
tumekuwa wagumu kubadilika kwasababu ya usahaulifu wetu. Leo hii mtanzania atalalamika kwa kukosa huduma za
msingi za kijamii ambazo mwakilishi wake alimuahidi atampatia pindi tu
atakapomchagua,lakini mwakilishi huyo huyo aliyeshindwa kutimiza ahadi zake ipo
siku atarudi tena kwa mtanzania huyo huyo na kumuomba kura huku akimuadaha na
maneno laini yanayosindikizwa na kanga,kitenge,kofia na shilingi elfu kumi,Hapo hapo mtanzania
huyo atasahau nini alikihitaji kutoka kwa kiongozi huyo,atasahau shida zote
alizozipata kwa miaka mingi na atauza kura yake kwa shilingi elfu kumi ya siku
moja bila kujali shida atazozipata kwa siku zaidi ya elfu moja.Huyo ndio
mtanzania.Ndio maana kila siku viongozi wetu ni wale wale na sisi tupo vile
vile hakuna mabadiliko.
Mwezi wa tano mwaka 2010 timu ya simba
ilifanya uchaguzi katika ukumbi wa bwalo la polisi oysterbay uliomuweka Aden rage kua mwenyekiti wa simba
kurithi nafasi ya Hassan dalali aliyemaliza muda wake, huku ndugu kaburu
akichaguliwa kua makamu mwenyekiti .Kabla ya hapo Aden rage aliwai kua makamu
mwenyekiti wa FAT pia katibu mkuu wa taasisi hiyo.Kwa ufupi aden rage hakuna
kipya alichofanya FAT.Lakini rage huyo huyo aliweza kurudi tena na kuwashawishi
wanasimba na kumpa ushindi wa
kishindo.Rage huyo huyo ndio aliyeongoza FAT iliyodumaa walimsindikiza kwa
nderemo na vifijo kuchukua fomu.Rage huyo huyo aliyefungwa kwa ubadhilifu wa
mali za fat ndio huyo huyo wakampa dhamana ya kulinda mali za simba. Ama kweli
binadamu tumeumbwa kusahau.Ila kama kusahau ni ugonjwa watanzania tunakaribia
kufa.
Siku
chache zijazo Simba itaingia kwenye uchaguzi
mkuu.Tumeona watu wanasindikizwa kuchukua fomu za kugombea uongozi wakisindikizwa na mavuvuzela.Ukipita kwenye
matawi huko ndo usiseme.Watu
wamecharuka,kila mtu na mgombea wake.Hivi ndivyo kampeni inavyokuwa. Nderemo
vifijo na shamrashamra kutoka kwa wagombea. Ila wapiga kura hao hao wengi wao
baada ya kupiga kura hujutia maamuzi yao.Hutamani siku zirudi nyuma watoe shilingi
kwa waliowapa kura zao.Lakini wakati uchaguzi ukifika tena hufanya makosa yale
yale ya kupiga kura kwa watu ambao si sahihi.
Zipo sababu
nyingi zinazosababisha watu kutofanya maamuzi sahii katika uchaguzi wa
viongozi.Lakini hizi ni sababu kuu zinazopelekea watu haswa wanachama wa vilabu
vyetu vikongwe kung’ata vidole vyao wenyewe wakati wa kupiga kura.
Kwanza ni kufuata
mkumbo,wapiga kura wengi haswa watanzania wanapiga kura kwa kufuata mkumbo.Wapiga
kura wengi ni wavivu wa kusikiliza na kuchambua sera makini za wagombea.Wapiga
kura wengi wanakosa taarifa muhimu za wagombea.Wapiga kura wengi wanaamini
kwenye maneno ya umbea,vijembe na majungu.Wengi wao wanapiga kura kwasababu ya fulani
kasema huyu anafaa na yule hafai.Ila ukimuuliza kwanini anafaa? au kwanini
hafai? hasilani hatakupa jibu sahihi.Kama mpiga kura inabidi usiwe mtu wa mkumbo.inabidi
ufanye upembuzi yakinifu kwa mgombea unayetaka kumpa dhamana ya
kukuongoza.Inabidi ujue kwanza alifanya nini bila kusahau anataka kufanya nini
na hiko anachotaka kufanya atakifanyaje?.Mpiga kura mwenye hekima ataachana na
stori za vijiweni na kutazama vitu hivi.
Imani
potofu ya mpira pesa,Siku hizi kuna maono mapya ya dunia. Ndani ya maono hayo kuna bosi mmoja tu. Bosi huyo ni pesa.Miaka
ya nyuma ili uheshimike kwenye jamii ilikua lazima uwe na Elimu,Hapo utashinda
dhidi ya umma. Maono mapya ya Dunia yanaamini mtu mwenye busara,Hekima na
kustahili Kuheshimiwa ni yule mwenye
pesa.uwe mwandisi,daktari,mwalimu bila shekeli hakuna atakayetambua na kuthamini
wala kuheshimu taaluma yako.
Kwenye Dunia yetu mpya
watu wameweka pesa mbele.Kinachonifurahisha zaidi hata kwenye ulimwengu wetu wa
soka pesa ndiyo inacheza mpira lakini watu wamesahau pesa hiyo hiyo ndio
inaharibu mpira.
Pesa si kila kitu
kwenye soka.”Heri masikini mwenye hekima kuliko tajiri mpumbavu”.Watu wengi
wenye pesa hupenda kuongoza timu kwa manufaa yao wenyewe.Ndio maana wengi wao
huzunguka mbuyu ili kuukwaa uongozi.Watu wengi wenye pesa huwa na malengo ya
kuongeza pesa zao kulilko kuitumikia timu.
Simba tangu ianzishwe imeongozwa na watu wenye pesa
wangapi? Na watu hao wenye pesa wameifanyia nini cha ziada wakati wa uongozi
wao zaidi ya kutunisha matumbo yao na kujiongezea umaarufu?
Wanachama wa simba
msiende mbali,muangalieni mtoto wa mama yenu wa kambo.Tangu mtoto wa mama yenu
wa kambo aongozwe na yule tajiri mwenye asili ya ki Asia wamepiga hatua gani ya ziada? Ndio wale wale
jana na leo na hata kesho watabaki vile vile japokua wamekubali kumuongezea
mwaka mmoja zaidi,lakini hakuna cha ziada atakachokifanya.Ahadi nyingi kubwa
aliahidi mpaka sasa hajatekeleza.
Najua mna mtihani wa
kuchagua kiongozi bora kwasababu viongozi wengi ni wale wale wa mwaka jana na
juzi,lakini kama hayupo bora basi atakuwepo kiongozi sahihi wa kuiongoza simba
kwa miaka minne ijayo.Nnachowasihi wanachama wa simba waache kufuata mkumbo,shirikisha ubongo wako.Usiuze kura yako
wala kuchagua kiongozi kwasababu ya pesa yake ambayo wewe hautakua na faida
nayo.Busara na hekima ndio sifa za kiongozi sahihi atakayewavusha salama miaka
hii minne.
By
Allen kaijage a.k.a middle ya juu
0655106767
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++


No comments