AZAM YAUA KAGAME CUP
> YAIBAMIZA MABINGWA WA ZANZIBAR KMKM BAO 4-0
.... mabingwa wa Tanzania watengeneza Ice Cream Azam FC jana waliinyuka KMKM ambao ni mabingwa wa Soka wa Zanzibar kwa bao 4-0 katika mchezo wa kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kagame Cup mchezo uliopigwa jana Jioni katika Dimba la Amahoro jijini kigali Rwanda.
Azam Fc ambao wamechukua Nafasi ya Yanga kuiwakilisha Tanzania Bara ilianza kuhesabu bao la kwanza dakika ya kwanza tu ya mchezo kwa kichwa maradhiwa cha Nahodha John Bocco kabla ya Prince Lionel hajafunga mengine mawili huku Bocco akimalizia la Nne na kuifanya Azam FC kuibuka na ushindi huo mnono.
Kwa matokeo hayo Azam FC wanaongoza Kundi A wakiwa na pointi 4 baada ya kucheza michezo miwili wanafatiwa na Rayon Sports yenye pointi 4 pia huku A-Almal ikishika nafasi ya 3, KMKM inakamata nafasi ya 4 ikiwa na pointi 1 huku Coffee ya Ethiopia ikikamata mkia.
Michezo mingine ya jana ilishuhudiwa Rayon Sports wakiifunga Coffee ya Ethiopia bao 2-1 wakati As Ali Sabieh ya Djibout iliifunga KCCA FC bao 2-1.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
No comments