TAARIFA ZA COSTA KWENDA CHELSEA NI UZUSHI ~ PEREZ


Raisi wa Atletico Madrid Enrique Perez amekanusha habari za Mshambuliaji wa timu hiyo Diego Costa kujiunga na Chelsea ya England na kusema taarifa zote zilizoripotiwa kuwa Costa amekamilisha vipimo vya afya ni uzushi.

Wiki hii kumeibuka taarifa nyingi hasa kutoka katika vyombo vya habari vya England zikisema kuwa Diego Costa ameshakamilisha utaratibu wa kujiunga na Chelsea na zoezi la upimaji wa afya limeshakamilika.



Diego Costa ambaye wakala wake ni yule yule wakala wa Kocha Jose Mourinho inasemekana amesaini kuichezea Chelsea kwa ada ya uhamisho wa Paundi milion 32 Wakati Perez yeye akisema atamruhusu mchezaji huyo kujiunga na timu yoyote anayotaka ikiwa ikiwa ataenda na kuzungumza hilo na uongozi kisha timu hiyo inayomtaka itoe ada ya uhamisho ambayo Atletico Madrid wanaamini inafikia Paundi milion 40.

Diego Costa mwenye umri wa miaka 25 amefunga 36 msimu ulioisha kwa klabu yake ya Atletico Madrid kiwango hicho cha magoli ni mara Tano ya magoli yaliyofungwa na washambuliaji wa Chelsea Samuel Eto'o, Demba Ba na Fernando Torres huku akiisaidia Atletico Madrid kushinda taji la La Liga baada ya kusotea kwa miaka 18 pia amekua muhimili mkuu wa timu hiyo na kuifikisha fainali ya Klabu Bingwa Ulaya ikipoteza kwa wapinzani zao wa jiji moja Real Madrid.


Hivi Sasa Costa yuko na timu yake ya Taifa ya Spain wakijiandaa na kombe la dunia huko Brazil licha ya kuandamwa na maunimvu ya misuli ya paja kila mara.

Licha ya Perez kukanusha kununuliwa kwa Costa lakini dalili zinaonyesha kabisa staa huyo atajiunga na Chelsea na pengine Chelsea wanaweza wakawasajili  beki wa Kushoto wa Atletico Madrid Felipe Luiz na kiungo Tiago.

Na Edo Daniel Chibo

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.