AC MILAN YAMTIMUA SEEDORF YAMTEUA PIPO INZAGHI



Wababe wa Soka la Ulaya wameendelea kuyumba baada ya kumtimua kocha wao ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa timu hiyo Clarence Seedorf huku wakitangaza nafasi hiyo sasa itakamatwa na mshambuliaji mwenye historia katika timu hiyo kwa miaka ya Nyuma Philipo "Pipo" Inzhagi.

Yani ni kama wametoa kiungo wameweka mshambuliaji baada ya wakali hao kuwahi kuichezea Milan wakiwa pamoja tena kwa mafanikio makubwa.

Clarence Seedorf alipewa kibarua cha kuinoa klabu hiyo kongwe mwezi January baada ya kutimuliwa aliyekus kocha mkuu wa timu hiyo Massimiliano Allegri.

Aliiongoza Milan katika michezo 22 na kushinda 11 tu huku Milan ikimaliza katika nafasi ya 8 katika msimamo wa ligi kuu nchini Italia maarufu kama Serie A.

Seedorf na Inzaghi wamecheza pamoja Milan wakati Seedorf akiwa kiungo huku Pippo akiwa mshambuliaji katika kikosi kilichokua tishio barani Ulaya.

Pippo Inzaghi anarudi Milan kama kocha mkuu katika mkataba utakaomweka hapo mpaka June 30,2016 akitokea katika kikosi cha vijana cha timu hiyo alichokua akikifundisha.

Unadhani hii inaweza kuwasaidia MILAN ambao wameanza kupotea katika ramani ya soka?

..Imeandaliwa na Edo Daniel Chibo

++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.