CESC FABREGAS "KUREJEA" LIGI KUU ENGLAND.

Cesc Fabregas

Ripoti kutoka nchini Hispania zinasema kiungo wa wakali wa Catalunha, Cesc Fabregas anajiandaa kuondoka klabuni hapo katika usajili wa majira ya joto msimu huu. Kituo cha  Habari za michezo cha Sky Sports wameripoti jana mchana kua kiungo huyo aliyewahi kuwa nahodha wa washika bunduki wa London, Arsenal anataka kurejea katika ligi kuu ya England na klabu ya Manchester United inatajwa kumwania mchezaji huyo ambaye amekosa maisha mazuri huko Catalunha.

Man United Itajaribu bahati yake tena msimu huu baada ya kushindwa kumsajili nyota huyo anayeimudu vyema nafasi ya Kiungo mkabaji. Aliyekua kocha mkuu wa Man United David Moyes alijaribu kwa kila hali kumsainisha lakini ilishindikana kutokana na Mchezaji mwenyewe kuonyesha nia kwa wakati huo. Inasemekana pia kocha mpya wa United Luis Van Gaal naye ameshaonyesha nia ya kumtaka nyota huyo japo haijathibitika rasmi lakini kwa kocha makini ambaye unatafuta kiungo huwezi kuacha kumtaja Cesc Fabregas.

Haitakua rahisi kwa United kumpata huyu jamaa kwani klabu iliyomlea Fabregas, Arsenal wanatajwa pia kuwa katika mipango ya chini chini ya kumrejesha kiungo huyo aliyewahi kuwatumikia kwa kipindi cha miaka 8 Ikumbukwe kua Arsenal wapo katika nafasi nzuri ya kumnasa tena nahodha wao huyo kwa bei chee iwapo tu watamhitaji kutokana na kipengele kilichowekwa katika mkataba wa mauzo yake mnamo mwaka 2012.

... By  Chardboy

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.