BAADA YA KUSTAAFU KUCHEZA SOKA PUYOL APATA KAZI NYINGINE BARCELONA
Aliyekua Nahodha wa Barcelona Carles Puyol ametunukiwa cheo cha makamu wa Mkurugenzi wa Michezo wa klabu ya Barcelona baada ya Kustaafu rasmi kucheza soka kutokana na maumivu ya goti aliyoyapata mwanzoni mwa msimu huu.
Puyol mwenye miaka 36 ametumia muda wake wote wa kusakata kabumbu akiwa na Barcelona na amecheza mechi 593 akiwa na klabu hiyo.
Puyol pia meshinda Ligi ya mabingwa barani Ulaya mara 3 na Ubingwa wa Ligi kuu Spain (La Liga) mara 6 akiwa na Barcelona akishinda pia kombe la dunia na lile la Ulaya akiwa na timu ya taifa ya Spain.
Puyol atakua akifanya kazi na Mkurugenzi mkuu wa michezo wa Klabu hiyo Andoni Zubizarreta kazi ambayo ataianza rasmi mwezi Septemba wakati msimu utakapoanza.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments