KWA TAARIFA YAKO ~ AZAM NDIYO KIRUTUBISHO SAHIHI KWA AFYA YA SOKA LA BONGO
Furaha ya watanzania wengi ni
kuona soka lao linakua,hakika mpira wa miguu ndio mchezo unaopendwa zaidi na watanzania.Japokua mchezo huu unapendwa
zaidi ila ndio mchezo unaowaboa na kuwakatisha
tamaa watanzania wengi.Timu zile
zile,viongozi walewale ,mawazo na malengo yaleyale.Kwa miaka kadhaa soka letu
limedumaa,kuanzia ngazi ya Taifa mpaka vilabu.Hii ni kutokana na kuwa na
viongozi wenye mawazo yaliyodumaa.
Simba na yanga ni moja ya
vyanzo vya kudumaa kwa soka letu.Timu
hizo kubwa kwa miaka mingi imekosa watu sahihi wa kuwafikisha kwenye hatma zao.Viongozi
wa simba na yanga wamekosa hekima na maarifa ya kuvipeleka vilabu hivyo
vinapopaswa viwe.Viongozi hao wameshindwa kutumia rasilimali watu kusukuma
gurudumu la maendeleo ya vilabu vyao.
Njoo unipe tofauti ya simba ya
karne ya 20 na simba hii ya leo.Hakuna jipya la kujivunia,simba ile ile ya
majengo pacha na makombe ya ligi kuu bara hakuna hatua yeyote waliopiga, huu ni
udumavu uliokithiri.Yanga ileile ya Kaunda hakuna la ziada.Hapa ndipo
tulipohitaji watu wenye maono mapya ili kuja kuwapa changamoto simba na yanga
zilizodumaa. Azam ni watu sahihi watakaotupeleka tunapotaka.Azam ni changamoto
sahihi kwa timu za simba na yanga .Azam ni kirutubisho sahihi kwa afya ya soka
la bongo.
Timu hii ya Azam iliyoanzishwa mwaka 2007 na wafanyakazi
wa kiwanda cha bakhresa kama timu ya mazoezi.Shukrani zimuendee Yusuph Bakhresa
aliyekuwa na maono ya kuwa na timu ya mashindano.Kwa hekima,maarifa na nguvu ya
pesa msimu wa mwaka 2008/09 Kwa mara ya
kwanza azam walishiriki ligi Kuu na kumaliza kwenye nafasi ya 8,msimu uliofuata
wakakamata nafasi ya tatu. Msimu uliyopita wakamaliza nafasi ya pili kabla ya
msimu huu wa mwaka 2013/14 kuibuka mabingwa wa ligi kuu vodacomna kujikatia tiketi ya
kushiriki kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika.Imechukua miaka saba(7) tu
kuchukua kombe la ligi tangu ilipoanzishwa.
Achana na simba na yanga zilizoanzishwa
karne ya 20 azam ina uwanja wa kisasa na academi bora kabisa ya soka nchini
bila kusahau gym na hostel za bei mbaya. Azam ni moja ya timu za kisasa Afrika
mashariki na kati.Mzee bakhresa ana dhamira na nia ya dhati ya kufanya yaliofanywa na kina moize katumbi
waTP mazembe Hakika Bakhresa Hajapoteza pesa zake
Ujio wa azam kwenye soka umeleta
faida kubwa tatu.Kwanza wamefanya ligi yetu kua bora na yenye mvuto,pili
imeleta changamoto kwenye timu ya Taifa na soka la Tanzania kwa ujumla, tatu
imesaidia kutangaza soka na ligi yetu nchi nzima.
Lakini leo ningependa
kuzungumzia nafasi ya azam fc kwenye ligi tu.
Ujio wa nguvu wa azam umetutoa
katika utawala wa Simba na yanga ulopelekea ligi yetu ikose mvuto na kusababisha watu kupoteza
hamu ya kupenda ligi yetu.Kadiri ya ligi inavyokua na timu zenye nguvu ndio
jinsi ligi inapokua na upinzani na kuitwa ligi bora.Unajua kwanini Ligi ya
uingereza inahesabika kua ligi bora?
Jibu ni hili Kabla ya Barclays
premier league mwaka 1992/93,mwaka mmoja
nyuma Arsenal na Liverpool walichuana vikali kugombea kombe la ligi,lakini
kwenye msimu wa kwanza wa Barclays ni Aston villa waliokua wanatishia ndoto za
Ferguson na watoto wake kuchukua kombe hilo kwa mara ya kwanza,kumbuka
Manchester united walikua wanasubilia kombe hilo kwa miaka 26,na Ferguson kwa
miaka 6,Manchester United waliwaacha Aston villa walioshika nafasi ya pili kwa
point 10 na kukata kiu yao,Huku Norwich city ikikamata nafasi ya tatu,msimu
uliofuata mambo yakawa tofauti kwa villa na norwich baada ya blackburn na the
magpies (Newcastle) kuwaondoa kwenye namba 2 na 3,Msimu wa mwaka 1994/95 mambo
yakawa tofauti si Manchester united, Leds,liverpool wala nottingham forest
aliyethubutu kuchukua kombe hilo mbele ya paka weusi(blackburn rovers),huku
allan shearer akifikia rekodi ya Andy cole ya kufunga magoli mengi kwenye
league kwa msimu mmoja magoli 34,na rekodi hiyo haijavunjwa mpaka hii leo.
Msimu
huo arsenal haikuwepo kabisa kwenye ramani ya washindani,lakini msimu unaofuata
(1995/96) ikaibuka kwa kushika nafasi ya nne na msimu unaofuata kukamata namba
tatu,kabla ya kuchukua ubingwa msimu wa mwaka 1997/98,Kipindi hiko Chelsea
haikuwa na upinzani mkali lakini ikaibuka na kuchukua kombe mara mbili 2004/05
na 2005/06.
Pia miaka hii mitatu manchester city ikaibuka na kutwaa kombe la
ligi mara mbili ndani ya miaka hii mitatu. Hapo utaona kupanda na kushuka kwa
timu nyingi sana.Ndani ya ligi kuna mechi nyingi ngumu na nzuri ukiacha mechi
za watani.Pia kwenye ligi hiyo kuna timu nyingi zenye uwezo wa kuchukua
ubingwa. Kwanini usipende ligi yao? Una kila sababu ya kuipenda.
Ukiacha uingereza iliyo bara lingine mfano
mzuri kwetu ni ligi ya Afrika kusini.Ligi hiyo imekua na timu nyingi nzuri
zenye ushindani.Mamelodi sundown,kaizer chief,Orlando pirates na super sport
united ni miongoni mwa timu zenye upinzani mkali.kati ya timu hizo yeyote
anaweza kua bingwa.Msimu huu kombe kachukua mamelodi msimu ujao anaweza chukua
Orlando pirates iliyoshika nafasi ya nne msimu huu.
Hapa kwetu Tanzania mwishoni mwa karne ya
20 iliibuka timu ya timu ya Mtibwa sugar na kutwaa ubingwa mara mbili mfululizo.Lakini mtibwa
haikudumu ikapoteza ubora wake kwa kuzidiwa nguvu na simba na yanga ikaja moro united,ikapotea.
Na sasa ni zamu ya Azam Fc ambayo mimi naamini ni timu sahihi iliojipanga
kuleta changamoto kwenye soka la bongo
Ujio wa azam umezifanya simba na
yanga zibadilike kutoka nafasi zilizozoea.msimu huu simba ameshika namba nne
hii imewapa fursa ya kujipanga vyema msimu ujao huku ikiwapa yanga onyo na
fundisho ya kua isipojipanga vyema msimu
ujao nayo itaaangukia pua.Hiki ndicho
tulichokuwa tunakisubiri miaka mingi kwenye ligi yetu.Hakuna mwenye nafasi yake
kwenye ligi,Usipojipanga unaambulia patupu,kila timu inavuna ilichokipanda
Licha
ya kuleta changamoto ndani ya uwanja ujio wa azam fc pia umewapa changamoto
simba na yanga zilizokaa miaka zaidi ya 70 bila kua na viwanja vyao binafsi na kuendesha akademi za
soka.Azam kwa miaka 7 wameweza kumiliki uwanja na kua na akademi bora ya
soka.Hapa wengi watasema azam wameweza kwasababu wanaongozwa na bilionea said
bakhresa,ni sawa lakini mimi naamini simba na yanga ni matajiri kuliko
azam,naamini simba na yanga zinaweza kua na viwanja bora kuliko chamanzi na
akademi bora kuliko ya azam kama wakipata watu sahihi wa kuwaongoza.Simba na
yanga zisiichukulie azam kama adui,bali waichukulie kama changamoto ya kujitoa
kutoka kwenye udumavu wao.
BY
kaijage jr(middle ya juu)
0655106767
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++



Umemaliza kila kitu middle ya juu.Biggie up!!
ReplyDelete