KOMBE LA FA LAMPA MKATABA WA MIAKA MITATU ARSENE WENGER

ARSENE WENGER


Baada ya tetesi za muda mrefu kuhusu mustakabali wa kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger kuhusu kuongeza mkataba ndani ya klabu hiyo hatimaye Mzee Wenger amesaini mkataba mpya utakaomweka Emirates mpaka mwaka 2017.

Mkataba huo umekuja baada ya neema ya kupata kombe la FA baada ya kukaa miaka 9 bila kombe ndani ya Emirates.
 Arsene Wenger mwenye miaka 64 alijiunga na Klabu hiyo ya London mwaka 1996 na kushinda mataji 8 mpaka sasa na anabaki kuwa kocha aliyedumu na timu moja kwa kipindi kirefu kuliko kocha mwingine yoyote katika Ligi kuu England kwa sasa.

Tangu Arsene Wenger alipojiunga na Arsenal timu hiyo haijawahi kukosa kushiriki Ligi ya mabingwa Ulaya kwa mwaka wa  17 mfululizo na huu ulikua ndo mwaka wa mwisho katika mkataba wake baada ya kujiunga na Arsenal akitokea China katika klabu ya Grampus Eight.

MAFANIKIO YA WENGER AKIWA ARSENAL
 
  • Premier League: 1998, 2002, 2004

  • FA Cup: 1998, 2002, 2003, 2005, 2014

  • Charity/Community Shield: 1998, 1999, 2002, 2004

  • Champions League runners-up: 2006

  • Uefa Cup runners-up: 2000

  • League Cup runners-up: 2007, 2011

  • +++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

    No comments

    Powered by Blogger.