KWA TAARIFA YAKO ~ AZAM NDIYO KIRUTUBISHO SAHIHI KWA AFYA YA SOKA LA BONGO



               Furaha ya watanzania wengi ni kuona soka lao linakua,hakika mpira wa miguu ndio mchezo unaopendwa zaidi  na watanzania.Japokua mchezo huu unapendwa zaidi ila ndio mchezo unaowaboa na kuwakatisha  tamaa  watanzania wengi.Timu zile zile,viongozi walewale ,mawazo na malengo yaleyale.Kwa miaka kadhaa soka letu limedumaa,kuanzia ngazi ya Taifa mpaka vilabu.Hii ni kutokana na kuwa na viongozi wenye mawazo yaliyodumaa.

               Simba na yanga ni moja ya vyanzo vya kudumaa kwa  soka letu.Timu hizo kubwa kwa miaka mingi imekosa watu sahihi wa kuwafikisha kwenye hatma zao.Viongozi wa simba na yanga wamekosa hekima na maarifa ya kuvipeleka vilabu hivyo vinapopaswa viwe.Viongozi hao wameshindwa kutumia rasilimali watu kusukuma gurudumu la maendeleo ya vilabu vyao.

                Njoo unipe tofauti ya simba ya karne ya 20 na simba hii ya leo.Hakuna jipya la kujivunia,simba ile ile ya majengo pacha na makombe ya ligi kuu bara hakuna hatua yeyote waliopiga, huu ni udumavu uliokithiri.Yanga ileile ya Kaunda hakuna la ziada.Hapa ndipo tulipohitaji watu wenye maono mapya ili kuja kuwapa changamoto simba na yanga zilizodumaa. Azam ni watu sahihi watakaotupeleka tunapotaka.Azam ni changamoto sahihi kwa timu za simba na yanga .Azam ni kirutubisho sahihi kwa afya ya soka la bongo.

                Timu hii ya Azam iliyoanzishwa mwaka 2007 na wafanyakazi wa kiwanda cha bakhresa kama timu ya mazoezi.Shukrani zimuendee Yusuph Bakhresa aliyekuwa na maono ya kuwa na timu ya mashindano.Kwa hekima,maarifa na nguvu ya pesa  msimu wa mwaka 2008/09 Kwa mara ya kwanza azam walishiriki ligi Kuu na kumaliza kwenye nafasi ya 8,msimu uliofuata wakakamata nafasi ya tatu. Msimu uliyopita wakamaliza nafasi ya pili kabla ya msimu huu wa mwaka 2013/14 kuibuka mabingwa  wa ligi kuu vodacomna kujikatia tiketi ya kushiriki kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika.Imechukua miaka saba(7) tu kuchukua kombe la ligi tangu ilipoanzishwa.
Achana na simba na yanga zilizoanzishwa karne ya 20 azam ina uwanja wa kisasa na academi bora kabisa ya soka nchini bila kusahau gym na hostel za bei mbaya. Azam ni moja ya timu za kisasa Afrika mashariki na kati.Mzee bakhresa ana dhamira na nia ya dhati  ya kufanya yaliofanywa na kina moize katumbi waTP mazembe Hakika Bakhresa Hajapoteza pesa zake

            Ujio wa azam kwenye soka umeleta faida kubwa tatu.Kwanza wamefanya ligi yetu kua bora na yenye mvuto,pili imeleta changamoto kwenye timu ya Taifa na soka la Tanzania kwa ujumla, tatu imesaidia kutangaza soka na ligi yetu nchi nzima.
Lakini leo ningependa kuzungumzia nafasi ya azam fc kwenye ligi tu.
                Ujio wa nguvu wa azam umetutoa katika utawala wa Simba na yanga ulopelekea  ligi yetu ikose mvuto na kusababisha watu kupoteza hamu ya kupenda ligi yetu.Kadiri ya ligi inavyokua na timu zenye nguvu ndio jinsi ligi inapokua na upinzani na kuitwa ligi bora.Unajua kwanini Ligi ya uingereza inahesabika kua ligi bora?

                Jibu ni hili Kabla ya Barclays premier league  mwaka 1992/93,mwaka mmoja nyuma Arsenal na Liverpool walichuana vikali kugombea kombe la ligi,lakini kwenye msimu wa kwanza wa Barclays ni Aston villa waliokua wanatishia ndoto za Ferguson na watoto wake kuchukua kombe hilo kwa mara ya kwanza,kumbuka Manchester united walikua wanasubilia kombe hilo kwa miaka 26,na Ferguson kwa miaka 6,Manchester United waliwaacha Aston villa walioshika nafasi ya pili kwa point 10 na kukata kiu yao,Huku Norwich city ikikamata nafasi ya tatu,msimu uliofuata mambo yakawa tofauti kwa villa na norwich baada ya blackburn na the magpies (Newcastle) kuwaondoa kwenye namba 2 na 3,Msimu wa mwaka 1994/95 mambo yakawa tofauti si Manchester united, Leds,liverpool wala nottingham forest aliyethubutu kuchukua kombe hilo mbele ya paka weusi(blackburn rovers),huku allan shearer akifikia rekodi ya Andy cole ya kufunga magoli mengi kwenye league kwa msimu mmoja magoli 34,na rekodi hiyo haijavunjwa mpaka hii leo.
Msimu huo arsenal haikuwepo kabisa kwenye ramani ya washindani,lakini msimu unaofuata (1995/96) ikaibuka kwa kushika nafasi ya nne na msimu unaofuata kukamata namba tatu,kabla ya kuchukua ubingwa msimu wa mwaka 1997/98,Kipindi hiko Chelsea haikuwa na upinzani mkali lakini ikaibuka na kuchukua kombe mara mbili 2004/05 na 2005/06.
 Pia miaka hii mitatu manchester city ikaibuka na kutwaa kombe la ligi mara mbili ndani ya miaka hii mitatu. Hapo utaona kupanda na kushuka kwa timu nyingi sana.Ndani ya ligi kuna mechi nyingi ngumu na nzuri ukiacha mechi za watani.Pia kwenye ligi hiyo kuna timu nyingi zenye uwezo wa kuchukua ubingwa. Kwanini usipende ligi yao? Una kila sababu ya kuipenda.

                 Ukiacha uingereza iliyo bara lingine mfano mzuri kwetu ni ligi ya Afrika kusini.Ligi hiyo imekua na timu nyingi nzuri zenye ushindani.Mamelodi sundown,kaizer chief,Orlando pirates na super sport united ni miongoni mwa timu zenye upinzani mkali.kati ya timu hizo yeyote anaweza kua bingwa.Msimu huu kombe kachukua mamelodi msimu ujao anaweza chukua Orlando pirates iliyoshika nafasi ya nne msimu huu.

                Hapa kwetu Tanzania mwishoni mwa karne ya 20 iliibuka timu ya timu ya Mtibwa sugar na kutwaa  ubingwa mara mbili mfululizo.Lakini mtibwa haikudumu ikapoteza ubora wake kwa kuzidiwa nguvu na simba na yanga ikaja moro united,ikapotea. Na sasa ni zamu ya Azam Fc ambayo mimi naamini ni timu sahihi iliojipanga kuleta changamoto kwenye soka la bongo

                  Ujio wa azam umezifanya simba na yanga zibadilike kutoka nafasi zilizozoea.msimu huu simba ameshika namba nne hii imewapa fursa ya kujipanga vyema msimu ujao huku ikiwapa yanga onyo na fundisho ya kua  isipojipanga vyema msimu ujao nayo  itaaangukia pua.Hiki ndicho tulichokuwa tunakisubiri miaka mingi kwenye ligi yetu.Hakuna mwenye nafasi yake kwenye ligi,Usipojipanga unaambulia patupu,kila timu inavuna ilichokipanda

               Licha ya kuleta changamoto ndani ya uwanja ujio wa azam fc pia umewapa changamoto simba na yanga zilizokaa miaka zaidi ya 70 bila kua na  viwanja vyao binafsi na kuendesha akademi za soka.Azam kwa miaka 7 wameweza kumiliki uwanja na kua na akademi bora ya soka.Hapa wengi watasema azam wameweza kwasababu wanaongozwa na bilionea said bakhresa,ni sawa lakini mimi naamini simba na yanga ni matajiri kuliko azam,naamini simba na yanga zinaweza kua na viwanja bora kuliko chamanzi na akademi bora kuliko ya azam kama wakipata watu sahihi wa kuwaongoza.Simba na yanga zisiichukulie azam kama adui,bali waichukulie kama changamoto ya kujitoa kutoka kwenye udumavu wao.

                                            BY kaijage jr(middle ya juu)

                                            kaijagejr@gmail.com

                                              0655106767

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
                                       

1 comment:

Powered by Blogger.