BRENDAN RODGERS NA MIAKA MIWILI YA MAFANIKIO LIVERPOOL

BR
Tarehe 1 June 2012 Klabu ya Liverpool ilimtangaza Brendan Rodgers kuwa kocha mkuu wa timu hiyo kufatia kuondoka kwa Kenny Daglish wiki mbili kabla na kumpa kandarasi ya miaka mitatu.
Rodgers mpaka anatangazwa kuwa kocha wa Liverpool alikua akiinoa klabu ya Swansea City inayoshiriki ligi kuu Engalnd.

Kufikia leo ni miaka miwili kamili tangu Liverpool walipoamua kumpa Rodgers kazi hii ya kurudisha makali ya Liverpool iliyokua tishio miaka ya Nyuma.

Katika msimu wake wa kwanza akiwa Liverpool Rodgers hakupata muda mwingi wa kuandaa mfumo wa soka lile analolitaka soka ambalo liliifanya Swansea City kuwa moto wa Koutea mbali mpaka kupewa jina la Swanselona ikifananishwa na klabu ya Barcelona ya Spain kwa staili yake ya Soka.
Liverpool ikiwa inakabiliwa na michuano mingi iliyopelekea kuwa na mechi nyingi zikiwemo zile za Kombe la Europa ilijikuta ikimaliza msimu huo wa Kwanza ikiwa nafasi ya 7 yani nafasi moja juu ya iliyoshika msimu uliotangulia.

Msimu wa mwaka 2013/2014 ulikua msimu wa Neema kwa Brendan Rodgers kwani alipata muda wa kuandaa timu iliyokua tishio katika ligi huku ikizidi malengo waliyojiwekea kwani Liverpool ilikua ni timu iliyokaribia kuchukua ubingwa wakati lengo ilikua kumaliza katika nafasi nne za juu ili kushiriki michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya.

Katika Misimu yake miwili Brendan Rodgers ameisaidia Liverpool kuibuka na ushindi mara 54 katika mechi 97 huku timu hiyo ikifunga jumla ya Magoli 208.

HONGERA BRENDAN RODGERS KAZI TUMEIONA

.....  By Edo Daniel Chibo 

No comments

Powered by Blogger.