NAHUSIKA NA UGONJWA WA RONALDO ~ MGANGA WA KIENYEJI
Katika hali isiyotegemewa mganga mmoja wa kienyeji nchini Ghana ametangaza kuhusika na Ugonjwa unaomsumbua staa wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo.
Zikiwa zimebakia siku 7 tu kabla ya kipenga hakijapilizwa huko Brazil kuashiria kuanza kwa Kombe la Dunia Cristiano Ronaldo ambaye ndiyo mchezaji bora kabisa wa dunia kwa sasa anasumbuliwa na maumivu ya goti huku madaktari wakijitahidi kila iwezekanavyo mkali huyo apone.
Mganga huyo anayejulikana kwa jina la Nana Kwaku Bonsam (Pichani) ametangaza kuhusika na ugonjwa huo na kudai hakuna hospitali yoyote itakayoweza kumtibu nyota huyo kwani ugonjwa alionao unatokana na maswala ya kiroho zaidi hivyo ni ngumu kuonekana.
Mganga huyo anasema ametengeneza Uchawi wa kumroga Ronaldo kwa kuwaua mbwa wanne wiki iliyopita. Anasema miezi minne iliyopita alisema kuwa atamfanya Ronaldo asicheze kombe la Dunia lakini hasa mechi dhidi ya Ghana na njia pekee ya kufanya hivyo ni kwa kupitia ugonjwa na ndicho alichofanya.
Ghana na Ureno zimepangwa kundi moja (Kundi G) katika fainali za mwaka huu na zinatarajiwa kukutana katika mchezo utakaopigwa tarehe 26 mwezi huu katika jiji la Brasilia
.... By Edo Daniel Chibo

No comments