LIVERPOOL YAKAMILISHA USAJILI WA RICKIE LAMERT WA SOUTHAMPTON
![]() |
| Rickie Lambert akiwa na Uzi wa Southampton |
Lambert mwenye umri wa miaka 32 alishawahi kuichezea Liverpool miaka mitano akiwa mchezaji Chipukizi kipindi ameanza kucheza soka, amezichezea pia Bristol Rovers,Stockport na Rochdale.
Msimu ulioisha katika ligi kuu Nchini England lambert amekua mhimili mkubwa wa kikosi cha Southampton baada ya kufunga magoli 14 akitoa pasi za mwisho 10 katika mechi 39 akitengeneza kombinesheni nzuri kati yake Adam Lallana na Jay Rodrigous.
Kama Kila kitu kikienda sawa basi Lambert atasafiri kuelekea Merseyside baada ya mechi ya leo Ijumaa ya kirafiki kati ya England dhidi ya Peru kupimwa afya na kutambulishwa Rasmi kama mchezaji wa Liverpool.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Hii Southampton itapukutishwa yote kwa wachezaji wao wote kusajiliwa na timu kubwa
ReplyDeleteKweli kabisa hawa south ya mtoni wanabomolewa bila huruma.
ReplyDelete