THE GUNNING MACHINE ~ LEO MWISHO WA UKAME?
Takribani miaka 9 sasa tangu kapteni Patrick Viera aliponyanyua kombe la FA katika uwanja wa Wembley kombe ambalo limeleta ukame wa makombe katika klabu ya Arsenal.
Enzi hizo kulikua na watu kama Ashley Cole,Kolo Toure, Lumberg,Pires,Henry,Berkamp na majembe mengi sana ambayo yaliweza kuipeleka Arsenal katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka uliofata na kufungwa na Barcelona
Leo hii Arsenal wanaikabili Hull City katika fainali za kombe la FA katika uwanja wa Wembley mechi itakayoanza saa 1 kamili jioni kwa masaa ya Afrika Mashariki.
Kila shabiki wa Arsenal anaamini leo ndo mwisho wa ukame wa makombe na mwanzo mpya wa makombe.
Kikosi cha hivi sasa kina vijana wengi sana tofauti na kile cha 2005. Mashabulizi leo yataongozwa na Podoski na Giroud
Wapo watu wanalidharau kombe hili lakini hili ni kombe lenye historia kubwa katika soka kwani ni kati ya mashindano machache yaliyoanzishwa miaka mingi sana iliyopita na hakuna kitu kizuri kama kulichukua kombe hili.
Sasa tuje katika mchezo husika leo dhidi Hull City. Arsenal imeshajihakikishia kucheza klabu bingwa Ulaya msimu ujao kwa kukamata nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi wakati Hull City wao wameshajihakikishia kucheza ligi ya Europa mwakani washinde leo au wafungwe na hii inatokana na nafasi ya Arsenal.
Thomas Vermaelen na Alex Oxlade Chamberlain ambao walikua majeruhi wanaweza kurudi leo kama vipimo vya afya vitawaruhusu.
Arsenal itaingia katika pambano la leo ikiwa kati ya hi chache kwa mwaka 2014 ambapo Kikosi kimekamilika ukiacha Theo Walcott na Serge Gnabry ambao majeruhi yao sio ya kupona hivi karibuni ila waliokua wagonjwa wote wako fiti hapa nawazungumzia Aaron Ramsey,Kieran Gibbs,Jack Wilshere na Abou Diaby.
Kitu kitakachompa shida leo ni kipa yupi ataanza kati ya kipa namba moja Wojciech Szczesny au kumwacha Lukas Fabianski ambaye ameibeba vilivyo Arsenal katika michuano hii ya kombe la FA.
Ukiacha fainali hii ambayo wengi tunaamini kua Wenger na Arsenal wanaenda kubeba kombe, Arsene Wenger amekua shujaa mara 4 kwa kunyanyua kombe hili yani mwaka 1998,2002,2003 na 2005.
Wenger amekaririwa akisema "Ukame wa makombe unaweza kufanya fainali ikawa ngumu kwa Arsenal lakini ukishakua uwanjani unabadilika kutokana na mchezo husika. Hutumii Historia kucheza ila unacheza kutokana na ubora wa kikosi, tunahitaji kucheza vizuri na kushinda"
FACTS
- Fainali ya leo ni ya 10 kwa kocha Arsene Wenger akiwa Arsenalna ni fainali ya 6 ya kombe la FA .
- Fainali ya leo ya kombe la FA ni ya 18 katika historia ya klabu hiyo na timu pekee iliyoweza kufikia namba hiyo ni Manchester United ambao nao wameshafika fainali 18 za kombe la FA.
- Katika fainali 18 hizo Arsenal imeshinda mara 10 timu iliyoshinda mara nyingi ni Man United ambao wameshinda mara 11.
- Katika Fainali 3 zilizopita za kombe la FA Arsenal haijaruhusu kufungwa goli.
- Hii ni mara ya kwanza kwa Hull City wakicheza fainali za kombe la FA na ibakua timu ya 57 tofauti kucheza fainali
Karibuni Wembley Kuwashuhudia Arsenal wakibeba kombe
Wembley Wembeley!!!!!
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++



No comments