TUNATAKA NYUMBA IMARA KWA MSINGI WA UDONGO MFINYAZI
Nilipokua mwanafunzi wa shule ya
msingi sikuwai ona umuhimu wake mpaka nilipo hitimu.Ungeniuliza kipindi hicho kwanini
nasoma shule ya msingi,Nisingekua na jibu la kukupa.Nilikua nikiona kama utaratibu
Fulani wa ukuaji wa mwanadamu. Sikuwai kufikiria kua siku moja elimu ya shule ya
msingi itanisaidia.Ilinichukua miaka saba tu kugundua siri iiliyofichika ndani ya
elimu ya msingi.
Ilikua kazi nyepesi sana kukabiliana
na masomo yangu ya sekondari kutokanana msingi imara niilotoka nao shule ya msingi,sikuhita
nguvu nyingi kwenda sambamba na masomo ya sekondari,Na siri kubwa ilikua ni msingi
imara nilioupata shuleya msingi.
Kilakitu bora huanza kwa msingi imara.
Ndugu yangu mwashi neno msingi si
neno geni kwake,Nyumba bora hujengwa kwenye msingi imara.Hata nyumba yenye wagivu
kwa rangi nzuri,bila msingi imara haiwezi kua nyumba bora.Ila nyumba bora
hukamilika kwa msingi imara.Nyumba imara hujengwa juu ya mwamba kama si nondo nzito
zinazoambatana na kokoto makini.Vitu vyote
hivi bora na imara huambatana sambamba na
muda bila kusahau gharama pia.
Kwa wale wenye haraka ya kuukimbia
muda na kukwepa gharama hutumia changarawe sambamba na udongo mfinyazi kama mbadala
wa kokoto ,Na matokeo yake baada ya kusimamisha jengo wanaingia gharama za kuziba
nyufa kila wakati na mwisho wa siku nyumba hiyo haidumu. Mwenye hekima atajenga
nyumba yake juu ya mwamba imara na kudumu nayo milele ila mpumbavu atajenga kwa
changarawe na kukaa nayo kwa miaka miwili kabla ya kujenga nyingine.
Waafrika wengi hasa Watanzania tunapenda
vitu vya harakahara na vya bei chee.Tunajali sana kumaliza kuliko kufanikisha.Kwenye kila sekta tumetawaliwa na pupa zinazopelekea tusifanikiwe.
Ebu nitoe king’ong’o nitumie mdomo kusema kitu
juu ya soka la bongo.Kila siku tumekua watu wenye kiu ya kufanikiwa lakini tunaishia
kuwa wahasidi.Tumekua kama wapumbavu tunaotaka mambo mazuri bila kufa kidogo. Tumekua
na husuda pasi nakujifunza.Kila siku tunasoma na kuona nchi zilizoendelea kisoka
zimefanya nini mpaka zimefika zilipo lakini hatutaki kujifunza katika mifano hiyo.
Tumefumbwa macho kwa ujinga kusubiri bahati
nasibu.
Mwaka jana
mwezi wa sita nilpata bahati kushuhudia baadhi ya mechi za umitashumta mjini
kibaha.Nilijionea hazina kubwa inayoenda kuliwa na tunutu.Bahati nzuri nzuri nilipata
kuongea na kocha wa timu ya taifa ya vijana wa chini ya umri wa miaka 15,Kocha
huyo alisema “tatizo la wachezaji wa Tanzania hawapati nafasi ya kukaa muda mrefu kwa pamoja tangu wakiwa na umri
mdogo, utakuta mtoto wa kwetu wa Denmark
na wa Tanzania wana vipaji sawa ila tofauti yetu inakuja onekana sababu ya wachezaji wetu kukakaa kwa muda mrefu kwenye akademi
za soka na kujifunza kucheza kitimu zaidi” hapo kocha huyo alimaanisha kua
Tanzania wanahitaji kujenga msingi imara wa soka kwa kuanzia kwenye akademi za
soka.
Maneno ya kocha huyo ni ukweli
mtupu,huwa sitaki kuamini kama wachezaji
wa ulaya wana vipaji vya ajabu ukilinganisha na wakwetu Afrika.Tofauti yetu ni
jinsi ya kutunza na kuendeleza vipaji
hivyo.Sammata angezaliwa Uingereza angekua anachezea Manchester united wakati
welbeck angezaliwa Tanzania angekua anachezea Tp mazembe.Hapo kilichobadilika
ni mahali mchezaji husika alipozaliwa tu.wakati webeck tangu akiwa na umri wa
miaka 11 akilelewa kwenye akademi za soka za Manchester united,sammata bila
shaka alikua akizunguka huku na kule na sembo mkononi kujaribu bahati yake
mitaani.Hili ni tatizo.Samaki mkunje angali mbichi,mchezaji mzuri hufunzwa
tangu utotoni.Inatubidi kua wavumilivu,tunahitaji kujitoa kwa muda na gharama
pia
Nikisema gharama utaniambia nchi
yetu ni maskini,Lakini kuna nchi masikini kama Tanzania tena nyingine ni
masikini zaidi ya Tanzania lakini
zimepiga hatua kubwa katika soka kuliko Tanzania.Angola ni moja ya nchi maskini
kuliko Tanzania lakini pamoja na
umaskini wao wamewai shiriki Kombe la Dunia huku Tanzania ikiangaika kila siku
kutafuta japo nafasi ya kushiriki AFCON bila mafanikio yeyote.
Nikikwambia muda utachoka
kusubiri huku ukiwaza kwenda Brazil kwa kambi ya wiki mbili wakati wengine waliandaa
timu ya kombe la Dunia miaka 10
iliyopita.Hapa hatuna ujanja zaidi ya kuwa wavumilivu,Senegal walivumilia
wakaweza,Spain walivumilia wakafanikiwa.Hakuna mchezaji hata mmoja wa kikosi
cha kwanza wa timu ya taifa ya spain ambaye hajapitia shule za mafunzo ya
soka.Na kikubwa zaidi hakuna hata mmoja kati ya wachezaji wa kikosi cha kwanza
cha spain ambaye hajapitia timu ya taifa ya vijana.Andres iniesta ambaye ni
moyo wa timu hiyo amechezea timu za vijana za madaraja yote tangu akiwa na umri
wa chini ya miaka 1
Nashukuru kwa maono mapya ya Tff
kuunda Timu ya taifa upya.Imethubutu kuzunguka kila mkoa kusaka vijana wenye
vipaji waliounda timu ya taifa mpya.Sina uhakika kama ni utaratibu mzuri
wametumia,sina uhakika kama mchezaji mzuri anatafutwa kwa njia walizotumia,Ila
nina uhakika wachezaji hao hawatoleta mabadiliko kwenye soka letu.Wengi wao
watakua wale wale aliosema kocha wa vijana.Hatuhitaji kuruka hatua
yeyote,tunahitaji kwenda ngazi kwa ngazi.Ili kujenga timu imara tunahitaji
kuanzia kwa wachezaji wanaotoka umitashumta
Umitashumta
itatupeleka kombe la Dunia kama sio Mataifa ya Afrika.Tuache mipango
yetu mifupi ya zimamoto na kuandaa
mipango ya miaka nane ijayo.Malinzi na Tff yake isifikiri kupata mafanikio
makubwa kwa muda waliopewa.Malinzi na
TFF kwa ujumla inabidi itujengee msingi Imara kupitia kutunza na kuendeleza
vipaji vinavyopatikana umitashumta.Kama vijana hao ambao wengi ni chini ya umri
wa miaka 15 watatunzwa na kuendelezwa tutaongea mengine baada ya miaka nane.Tff
inabidi iwekeze zaidi kwenye umitashumta
ili kujenga msingi imara wa soka la Tanzania kwa miaka mingi ijayo.
Imeandikwa
na
Kaijage jr(middle ya juu)
kaijagejr@gmail .com,0655106767


No comments