UPAMBE WA KAIJAGE KWENYE HARUSI YA KISPANYOLA, ZURICH. SEHEMU YA PILI (2)
entebila. Bar hyo
ilikua ikiitwa lujan pub. Lujan pub ilikua ikimilikiwa na mzee lujan
baba mzazi wa jose antonio. Mzee lujan umri ukamtupa mkono na kuwaachia
watoto wake wawili wa kiume Jose antonio na kaka yake.,waendelee
kusukuma gurudumu la lujan pub. Familia ya mzee lujan macho yao yote
yalikua yanatazama lujan pub kama mkombozi pekee wa maisha yao..
Mwanzoni mwa miaka ya 1980's Antonio reyes akapata mwanamama
aliyejulikana kwa jina moja la Maria. Mnamo mwaka 1984 wakapata mtoto wa
kiume aliyejulikana kwa jina la Andres Iniesta Lujan.. Hyo ilikua miaka
9 tangu lujan pub izaliwe.. Kaya ya lujan ikawa na jumla ya watu nane
baada ya kuzaliwa kwa dada wa iniesta aitwaye Maribel.. Jose antonio
kama kiongozi wa familia akapanga zamu ya kila mwana familia kukaa
counter pale lujan pub.. Lakin ilipokua inafika zamu ya andres, muda huo
tayari alikua alishafika kwenye viwanja vya la mancha.. Mzee jose
antonio alitumia maneno yote ya kamusi ya kispanyola kumkanya juu ya
ukaidi wake.. Lakini bahati mbaya alikua akimpigia mbuz gitaa. Ndo
kwanza mjukuu wa lujan akasajiliwa kwenye timu ya vijana ya albacete
iliyopo mjini fuentabila.. Mzee antonio akapingana na matamanio yake kwa
ajili ya kutimiza hatma ya mtoto wake pekee wa kiume.. Andres alipofika
umri wa miaka 12,wazaz wake wakampeleka kwenye kituo cha soka cha la
masia mjini barcelona. Huu ndo ulikua mwanzo wa mafanikio ya mjukuu wa
lujan.. Andres iniesta amecheza kwenye timu zote za taifa. Mpaka kufikia
kipindi hiki andres iniesta mwenye kilo 65 tu zinazowalambisha majani
viungo wengi ulaya, amepata mafanikio mengi ya kukumbukwa kwenye timu ya
taifa na club yake ya fc Barcelona.. 2achane na mavi ya kale.. Je
andres alifanya nini ndani ya mwaka huu mpaka awe na sifa ya kua bwana
harusi mnamo january kwenye mji wa zurich
Mafanikio ya Andres Iniesta mwaka 2011/12
BARCELONA- Copa del rey
Spanish supa copa
8 Goals and 7 Assists.
SPAIN- Uefa European Champions
2 goals, 2 assists
INDIVIDUAL-
Europe best player
Allen hivi unadhani huyu jamaa atashinda tuzo ya mwanasoka bora wa dunia kwa hizi rekodi za Messi?
ReplyDelete