NAMSHUKURU MUNGU NILIKUWEPO WAKATI REKODI HIZI ZIKIWEKWA
Kuna Rekodi nyingi zinawekwa duniani siku za hivi karibuni ambazo watu wengi waliokwisha kutangulia mbele ya haki walitamani kuzishuhudia lakini Mungu hakuwapa fursa hiyo
Ukiangalia Rekodi anazovunja Usain Bolt katika kufukuza upepo utaamini haya ninayoyasema hapa na mara nyingi najiuliza hivi atakuja kutokea mtu wa kumzidi huyu jamaa? Natamani nije kumwona huyo mtu.
BAADHI YA REKODI ZA HIVI KARIBUNI KATIKA SOKA
Katika Soka (kandanda) zipo rekodi nyingi zimewekwa siku za hivi karibuni ili kuzifunika zile za zamani au kuweka rekodi mpya na huu ndo utamu wa michezo hasa kandanda ambao ndo mchezo unaopendwa zaidi kwa sasa duniani na nadhani itabaki kua hivyo milele.
Hebu tuangalie baadhi ya rekodi hapa katika Soka au Kandanda
- Kikosi cha Arsenal cha msimu wa mwaka 2003/2004 kama kinavyoonekana katika picha juu ndo kikosi pekee katika Ligi kuu England kumaliza msimu mzima bila kupoteza mchezo wowote wakivunja rekodi iliyowekwa na Preston North End mwaka 1889.
- Msimu wa mwaka 2011/2012 Katika Ligi kuu England kumeshuhudiwa timu kubwa zikifungwa magoli mengi hasa yaliyovunja rekodi ni Man United 8-2 halafu ikaja Man United 1-6 Man City hii inaingia katika rekodi muhimu.
- Kwa mara ya kwanza katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Ikashuhudiwa Bingwa mtetezi Chelsea akitolewa katika hatua ya makundi na hii imetokea msimu huu 2012/2013
- Man City imeweka rekodi ya kua timu pekee kutoka EPL kutoshinda mchezo wowote katika raundi ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu wa 2012/2013
MESSI NA REKODI YA GERD MULLER
Najua zipo rekodi nyingi kutoka sehemu mbalimbali lakini lengo ni kuzungumzia REKODI iliyowekwa miaka 40 iliyopita na gwiji la soka la Ujerumani na timu ya Bayen Munich Gerd Muller.
Imeshuhudiwa katika usiku wa tarehe 9/12/2012 Kijana kutoka Argentina anayekipiga katika Club ya Barcelona ya Hispania akijulikana kwa jina la Lionel Andres Messi. Messi ana miaka 25 bado ana mengi ya kuyafanya katika soka
"Hata kama humpendi au humkubali basi shukuru Mungu umeshuhudia rekodi ikivunjwa jifanye kama humjui aliyeivunja"
No comments