THE GUNNING MACHINE
ARSENE WENGER NA MAAJABU YAKE NDANI YA ARSENAL
SEHEMU YA 2
![]() |
Uwanja wa zamani wa Arsenal- Highbury |
Baada ya Arsenal kupokwa ubingwa wa wa ligi kuu na Man UTD katika msimu wa mwaka 2002/2003 huku wakifanikiwa kutetea kombe la FA, Tunaendelea kutazama maajabu ya Wenger katika misimu iliyofuata.
Msimu wa 2003/2004,yale aliyoyasema yalitimia.maajabu mengine ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu bila kupoteza mchezo wowote.arsenal wakaenda na mwendo mzuri katika EPL kwa mechi 49,lakini bahati mbaya mechi ya 50 ikaangukia kwa Manchester UTD na wakaimaliza rekodi hiyo murua ya arsenal kwa kichapo cha 2-0 October 2004.
Invinsible Arsenal
Katika msimu huo wa 2004/2005 Arsenal walimaliza katika nafasi ya 2 nyuma ya chelsea. Lakini Wenger akajitahidi kuendeleza maajabu yake kwa kutwaa kombe la FA mbele ya Man UTD kwa matuta.
Baada ya hapo maajabu yakawa ni anguko la ghafla la Arsenal katika misimu ya 2005-06 na 2006-07 wakishika nafasi ya 4 ktk ligi huku wachezaji wao nguli wakitimka.
Pamoja na hayo,Wenger alitaka kuandika maajabu mengine katika soka baada ya kuifikisha Arsenal fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya May 2006 wakicheza michezo 8 bila kuruhusu goli,lakini kadi nyekundu ya golikipa Jens Lehman ktk mchezo wa fainali dhidi ya barcelona ukawaua arsenal baada ya Barcelona kutoka nyuma ya 1-0 mpaka kushinda 1-2 katika dakika 15 za mwisho.
Jens Lehman akitolewa kwa kadi nyekundu
Ni katika mwaka huo 2006 ndipo Arsenal walipohamia katika uwanja wao wa Emirates ambao ulikua wazo wa Wenger la siku nyingi kwamba 'club kubwa inahitaji uwanja mkubwa'
Wenger alitaka kujaribu kutwaa kombe la carling mwaka 2007 lakini akataka kufanya maajabu kwa kutumia kikosi cha vijana dhidi ya chelsea,akaishia kupoteza 2-1 ktk fainali.
Wenger akasaini mkataba mwingine September 2007 ambao mwenyewe aliuita 'commitment to the club of my life'.
Katika msimu huo wa 2007-08,alitaka kufanya maajabu mengine baada ya kuiongoza Arsenal kuwa club ya kwanza kufikisha point 60 mwezi februari.lakini msimu ukaharibiwa na majeruhi ya wachezaji tegemeo huku kubwa ikiwa ni majeruhi mbaya ya mshambuliaji Eduardo ambayo iliwatoa wachezaji kisaikolojia na hivo kupata sare 3 mfululizo ambazo ziliwapa nafasi Chelsea na Man UTD kuisukuma Arsenal katika nafasi ya 3.
Msimu wa 2008-09,Arsenal waliuanza vibaya,wakiwa wamewauza Mathieu Flamini,Gilberto Silva na Alexander Hleb.walimaliza katika nafasi ya 4 pamoja na kufika nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya na kombe la FA.Ndipo mtu huyu wa maajabu alipoanza kushutumiwa vikali.
Msimu wa 2009-10,timu ikamaliza katika nafasi ya 3 huku wakiaibishwa na Barcelona kwenye robo fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya .Lionel Messi akifanya vitu adimu sana kwenye soka usiku huo.
Wenger akakaribia kukata kiu ya vikombe msimu wa 2010-11,lakini makosa ya beki Laurent Koscienly na golikipa Wojciech Szczesny yakampa nafasi Obafemi Martins kuwafunga Arsenal ktk fainali na kuwakosesha kombe la Carling ambalo walilihitaji sana.hali ya hewa ikachafuka na wakamaliza katika nafasi ya 4 EPL.
Mwaka 2011-12,Wenger akawauza nahodha Cesc Fabregas na Samir Nasri.kikosi kikawa dhaifu sana, ukiongeza Suspensions na injuries vikapelekea kipigo kikali cha mabao 8-2 kutoka Man UTD August 29,2011. Wakamaliza katika nafasi ya 3 huku nahodha Robin Van Persie akifunga magoli 37.
Nahodha huyo tegemeo akauzwa kwenda Man UTD ktk msimu wa 2012-13 huku Wenger akikiri kuwa amewanunua Olivier Giroud na Lucas Podolski kuziba nafasi yake.Msimu unaendelea na wakati naandika makala hii,arsenal chini ya mtu huyu wa maajabu inashika nafasi ya 10 kwenye ligi na tayari imekata tiketi ya kucheza 16 bora katika Champions League.
Mkataba wa mfaransa huyu una mwaka mmoja tu (2013) kukamilika,je ataendelea kuwepo Kwa kipindi kingine?
Hatujui kwa sasa ila tutaona pamoja na kupitia The Gunning Machine tutatafakari pamoja.
Hayo ndiyo maajabu ya Arsene Wenger katika club ya Arsenal.
Tukutane tena Mwishoni mwa wiki.
Imeandikwa na Richard Leonce ChardBoy kutoka Wapenda Soka 'Kandanda' group katika mtandao wa facebook
No comments