NGASSA KUZIPIGA CHENGA AZAM,SIMBA NA EL-MEREIKH KISHA KUSAINI YANGA NI UJANJA?

                                                                   Mrisho Ngassa
Hapo jana msemaji mkuu wa timu ya El Mereikh ya Sudan alikaririwa akisema Wametoa siku moja kwa mchezaji wa Azam Fc anayeichezea Simba ya Dar es Salaam Mrissho Khalfan Ngassa (pichani) kujitokeza na kusaini au kukataa kusaini formu za kukipiga na timu hiyo baada ya kukubaliana mwanzoni,
Ngassa mwenyewe akiwa mafichoni alinukuliwa hiyo hiyo jana akikana kukutana na wawakilishi wa timu hiyo na kutokua tayari kwenda Sudan kucheza soka la kulipwa.
                                               Ngassa akikabana na Fabio wa Man United

Leo zimekuja taarifa mpya kabisa na kuthibitishwa na baadhi ya viongozi wa yanga kuwa Ngassa ameshamwaga wino wa kuichezea klabu hiyo ya Jangwani ambayo hivi sasa iko chini ya Mwenyekiti Tajiri  Yusuph Manji
Ngassa na Manji
"Ni kweli Ngassa amesaini Pre Contract na Mabingwa wa Kagame Yanga mkataba wa miaka miwili na ameshakabidhiwa kiasi cha milioni 10 na fedha nyingine atamaliziwa mara atakapomaliza mkataba wake wa kuichezea Simbamwishoni mwa msimu huu" kilieleza chanzo hicho.
Kwa sasa mshambuliaji huyo wa kutumainiwa wa klabu ya Simba na timu ya Taifa ya Tanzania mabae alimaliza akiwa juu katika kupachika mabao katika michuano ya Challenge iliyomalizika hivi karibuni nchini Uganda, haonekani na hapatikani katika simu kwa wiki nzima sasa na hakuna anayejua alipo kwa upande wa vyombo vya habari.
Kupitia kwa msemaji wake El Mereikh walikubaliana na Simba na Azam ambao ni wamiliki wa mchezaji huyo kwa sasa kuwa italipa dola 100,00 makisio ya milioni 15 za kiTanzania huku mrisho Ngassa akipewa dola 75,000 makisio ya milion 110 za kiTanzania huku Akipewa mshahara wa dola 4,000 makisio ya milion 6 za kitanzania kwa mwezi.

Habari ndani ya klabu ya Simba zinasema Viongozi wanaendelea na mazungumzo ya kuwashawishi El Mereikh wamchukue Kiungo mshambuliaji wa timu hiyo na Timu ya Taifa ya Tanzania Mwinyi Kazimoto baada ya Jaribio lao( El Mereikh) la kumnasa Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima kugonga mwamba baada ya mchezaji huyo kusema atabaki na Timu yake ya Yanga.
                                                               Mwinyi Kazimoto

KAMA MDAU WA SOKA UNAONAJE JAMBO HILI?


>>>>>>>>>>>>Habari hii imeletwa na Bab Chicharito wa wapenda Soka (kandanda) group katika facebook<<<<<

9 comments:

  1. Dah mpira wa Tz full vituko, me sielewi taratibu zinakwendaje, nasubiri kuona picha itakapoishia!

    ReplyDelete
  2. Bhangi
    mademu
    ndumba
    kuuza mechi
    kuifunga Simba
    ndo sababu tosha hizo za maamuzi ya kipuuzi kama haya kamwe hatuwezi kuendelea

    ReplyDelete
  3. kIla mwanadamu mwenye akili timamu anafanya THE BEST ALTENATIVE CHOICE... MONEY CANT BUY HAPINESS.... HATA MPUTU ALISHAWAHI GOMA KWENDA ARSENAL AKABAKI MAZEMBE COZ IS WHERE HAPINESS IS.

    ReplyDelete
  4. Hahhahahaahaah eti Money cant buy Happines
    Pesa kila kitu jama huxu jamaa elimu ndogo na kua na washauri wajinga ndo kumemcost
    El Mereicky ni level za TP Mazembe huwezi ukanambia hawezi kua happy hapo na wakati Samatta anaenda Mazembe wapo watu waliokua na maslahi binafsi walimtaka abaki Simba na yeye kwakua baba yake ameelimika alilipinga hilo na kung'ang'ania mwanae aende CONGO angalia sasa dogo ananunua tu maviwanja mbagala huko na mwakani anakuja kuoa hiyo ndo discipline
    Hawa wakina Ngassa mabangi yanawasumbua na issue za kupenda sifa pia wakati umri unasogea

    ReplyDelete
  5. Hiki kitendawili sasa, Ngasa inasemekana anasema yeye hajawahi kukutana na hao jamaa na hinyo hawezi kwenda huko kwa kuwa hajashirikishwa, El Meleikh nao wanasema walishakutana na Ngasa wakaongea nae na wakaelewana na Ngasa mwenyewe ndio alewaambia waje waonane na Azam na Simba. Dah sasa hapo sijui nani mkweli!!!

    ReplyDelete
  6. Bt me sion kosa!kwan kusign yanga kosa??kafata moyo wake unachotaka...good 4him hajatamani pesa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. fikiria mara mbili au ikiwezekana zaidi ya hiyo fikira yako then njoo unipe jibu

      Delete
  7. fitna za kijinga, washauri wabovu, ushabiki wa kipumbavu, umalaya na sifa za kijinga plus bangi ndo matokeo ya haya madudu eti kafuata happy ni umbumbumbu

    ReplyDelete
  8. happiness ni kuchezea Yanga?
    Duuuuh hii kali

    ReplyDelete

Powered by Blogger.