MACHOZI YA SOKA LETU BONGO
siku ya kwanza kutumika uwanja mpya katika mechi |
Ni Jioni ya jumapili moja katika moja ya meza za Pub maarufu sana kwa wapenda soka maeneo ya Ubungo External jijini Dar es Salaam kulikua na watu wawili wakipiga story zao huku wakitazama mechi ya EPL kati ya West Ham na Liverpool kwenye luninga .watu hao si wengine ni mimi Chardboy,mhariri wangu Edo Daniel Chibo na katikati yetu alikuwepo mpambe Allen Kaijage.
Katikati ya mazungumzo,tukajikuta tunalizungumzia soka la bongo.Allen Kaijage ambaye ni kijana mdogo tu,tena msomi na mpenzi wa mpira akasema bila aibu kwamba yeye hana habari kabisa na soka la hapa ingawa anawajua wachezaji na baadhi ni rafiki zake.
Mimi nikacheka kidogo,sikucheka kwa furaha,la nilicheka tu kunogesha mazungumzo kisha tukaendelea na stori zetu.kichwani mwangu nikaanza kufikiria mambo mengi sana,fikra zangu zikaanza kuitafuta sababu ya Allen kutopenda soka la bongo. Allen ni mpenzi wa Arsenal,wote tunajua Arsenal haifanyi vizuri kwa kipindi sasa. Je ni kwa nini Allen anaipenda Arsenal wakati haipendi Simba? Zingatia kua akina Ramadhan Chombo ni washkaji zake lakini hajawahi kumwona Tom Rosicky!
Nisiache boriti jichoni mwangu,nikaamua kulipiga picha soka letu ili nione kama linatabasamu lakini bahati mbaya nikalikuta linalia,tena linalia machozi.
Nikakumbuka tangu mimi naanza kupenda mpira zamani kabisa kwa umri wangu.niliipenda yanga ikiwa na kocha mzungu Mc Lennan mwaka 1997,wakamtimua tu bila sababu za msingi wakampa timu marehemu Tito Mwaluvanda.

Mungu si Athumani,Mwaluvanda ambaye alikua amepewa timu kwa muda tu akachukua ubingwa wa bara kwa kuweka rekodi ya ushindi mkubwa katika ligi hiyo wa 8-0 dhidi ya Kagera Stars,Lunyamila anapiga 5 peke yake.Lunyamila alikua kama Messi bwana.
Akamzodoa kocha wa kagera,Zacharia Kinanda ambaye alikua ndo kocha wa Taifa Stars huku akimkataa Lunyamila kwenye timu yake.
Basi Mwaluvanda akaifikisha Yanga hatua ya makundi ligi ya Mabingwa Afrika.alipowafikisha hapo tu akatimuliwa,nafasi yake akapewa Raoul Shungu.ajabu ni kuwa mpaka kufika hapo yanga iliitoa Rayon ya Rwanda ikiwa chini ya Shungu!
Basi soka yetu ikalia machozi ya kwanza mimi nikishuhudia na akina Kaijage wengi wakalikimbia.
Nikamkumbuka Alex Kajumulo ambaye alikuja na Mipango safi katika Soka yetu,lakini akakatishwa tamaa,nae akakata tamaa akalitosa soka letu,likalia machozi mengine na akina Kaijage wengine wakaondoka zao.

Hiyo ni mifano tu,yapo mengi sana yakaendelea kuwafukuza akina Kaijage kwenye soka letu.
Nikaikumbuka Simba ya James Siang'a akiwa na akina Juma Kaseja,Boniface Pawasa,Patrick Betwel,Nico Nyagawa,Joseph Kaniki,Ulimboka Mwakingwe na wenzao walivoitikisa Afrika kabla ya Kutimuliwa Siang'a na kuiliza machozi mengine soka yetu.
Narudi nyuma kwa ile Yanga ya kina Manyika,Said Mwamba,Chibe Chibindu,Ali Mayai,Mohamed Hussen na Lunyamila ilivotisha ktk ukanda huu.kuna stori kwamba Lunyamila alimpiga chenga mtu mmoja anaitwa Poa Sule akavunjika kiuno na hajarudi uwanjani hadi leo.sijui kama ni kweli.
Kipaji cha Lunya akiwa na klabu ya Yanga
Nikakumbuka ukasuku wetu kwamba tunahitaji vijana sasa.Tukaipenda kwa moyo wote Serengeti Boys ya kina Yusuph Mgwao,Nizar,Tegete na Mrope.lakini tukapenyeza kijeba Nurdin Bakari tukapoteza nafasi yetu.soka ililia sana wkt huo na akina Kaijaege wengine wakapotea.
Nikazitazama zama hizi za akina Samatta,Domayo,Msuva,Singano na Mkude. Nikajitazama mimi nikagundua vitu vingi sana vingi sana vimebadilika.tuna uwanja mpya,mikataba mizuri ya wachezaji,udhamini wa kueleweka wa timu ya Taifa na Mengine ambayo ni masharti tu ya nyakati.kuna wakati unafika unahitaji vitu hvyo.
Lakini nikaumia sana kuona soka letu bado linalia machozi.Tangu enzi zile mimi nasoma Chekechea pale Mafumbo Bukoba,mpaka sasa nafanya kazi bado soka linalia machozi yale yale tu.

Taifa Stars ya zamani wakiwa vifua wazi kabla ya mechi na Sudan
Wakati nawaona akina Doyi Moke na Sekilojo wakicheza na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini miaka hyo,wanafungwa lakini wanatoa upinzani,nilidhani ipo siku tutasimama nao level moja,kumbe wapi!
Sundowns ya leo imekua kubwa sana kuliko Yanga ya leo.yanga bado inalia vile vile kwa sauti ile ile.kilichobadilika ni masharti ya nyakati tu.

Nainua macho yangu kuyapeleka kwenye luninga kuitazama Liverpool mbovu kuliko liverpool zote kuwahi kuziona,lakini naiona imeendelea sana kuliko ile ya kina John Barnes.Maendeleo yake yanaonekana pamoja na kua haichezi vizuri kwa sasa.
Leeds UTD ya England ambayo ilishashuka daraja inaweza kua na maendeleo kuliko Yanga ya sasa.
Ligi yetu sisi hata kuiona kwenye luninga ni bahati tu.
Watu watasema siyo sahihi kulinganisha soka letu na ulaya,na mimi nitawauliza kwani soka lina ukabila?
Kuna mchambuzi mmoja aliwahi kunambia Hamis Gaga alikua mzuri kuliko Zidane,siwezi kumbishia,hata mimi najua kua Samatta ni mzuri kuliko Chammackh.
Hamis Gaga wa kwanza kushoto
Lakini kinachouma ni kuona soka la Chammackh linacheka na la Samatta linalia,Chammackh anaweza kumdanganya mtoto wake kwamba 'mimi nilikua bonge la striker' na akaaminika.kweli Kaijage alikimbia machozi.
Taifa Stars ya sasa
Imeandikwa na Richard Leonce Chardboy kutoka group la Wapenda Soka(kandanda).
Ungana nami kupitia chardboy77@yahoo.com Au 0658399341

Mmmh!
ReplyDeleteAbel nini tena?
ReplyDeleteDah! hiyo picha ya stars wapo vifua wazi imeniacha hoi
ReplyDelete