YANGA YAIKOSA RASMI SAFARI YA UINGEREZA
Rasmi Yanga imekosa tiketi ya kwenda Uingereza kucheza na klabu ya Everton baada kutupwa nje ya michuano ya SportPesa Super Cup inayoendelea nchini Kenya.
Bingwa wa michuano hiyo inayo shirikisha timu nane kutoka Tanzania na Kenya atasafiri kwenda Uingereza kucheza na Everton katika uwanja wa Godson Park.
Hata hivyo Yanga ilikuwa haipewi nafasi ya kufanya vizuri katika mashindano hayo kutoka na kuaacha baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza wakiwemo walinzi wa kati Kelvin Yondani na Vincent Andrew 'Dante'.
Kakamega walipata mabao mawili ya haraka dakika za 25 na 30 kupitia kwa mshambuliaji Allan Wanga huku la pili likiwa la mkwaju wa penati.
Matheo Anthony aliifungia Yanga bao hilo pekee kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja dakika ya 38.
Wycliffe Opondo alipigilia msumari wa mwisho kwa Yanga baada ya kufunga bao la tatu dakika ya 85 kufuatia uzembe wa wachezaji wa mabing hao wa zamani wa bara.
Katika mchezo wa pili ambao upo mapumziko muda huu mabingwa watetezi Gor Mahia wapo mbele kwa mabao 2-0 dhidi ya JKU.

No comments