GOR MAHIA NAYO YATINGA NUSU FAINALI SPORTPESA SUPER CUP
Mabingwa watetezi wa michuano ya SportPesa Super Cup timu ya Gor mahia imeingia nusu fainali ya mashindano hayo kufuatia kuifunga JKU mabao 3-0.
Gor imekuwa timu ya pili kutoka Kenya kuingia nusu fainali ya michuano hiyo baada ya Kakamega Homeboyz kufanya hivyo kwa kuifunga Yanga mabao 3-1.
Mabingwa hao walienda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao mawili yaliyofungwa na George Othiambo 'Blackberry' dakika ya 30 na Godfrey Walusimbi dakika ya 36.
Kabla ya Odhiambo kufunga bao hilo alipoteza mkwaju wa penati dakika ya 22 baada ya mlinzi wa JKU kufanya madhambi ndani ya 18.
Mfungaji bora wa michuano hiyo msimu uliopita Meddy Kagere aliifungia Gor bao la tatu kwa kichwa dakika ya 71 baada ya kumalizia mpira wa krosi kutoka upande wa kulia.
JKU imeungana na Yanga kukusanya virago kurejea nyumbani baada ya kukubali vipigo hivyo.
Wawakilishi wengine wa Tanzania timu za Simba na United zitashuka dimbani kesho kucheza dhidi ya Sharks na AFC Leopards.

No comments